MEE: Saud Arabia inafadhili kampeni za uchaguzi za Clinton
Kituo cha habari cha Middle East Eye (MEE) cha Uingereza kimefichua kuwa Saudi Arabia ni miongoni mwa wafadhili wakuu wa kampeni za uchaguzi za mgombea wa kiti cha rais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democtatic, Hillary Clinton.
Middle East Eye imeripoti kuwa, Naibu wa Mrithi wa Kiti cha Ufalme cha Saudi Arabia, Muhammad bin Salman amesema, Riyadh imetoa asilimia 20 ya gharama za kampeni za uchaguzi za Hillary Clinton.
Hii ni pamoja na kuwa ni kinyume cha sheria kwa kampeni za uchaguzi za mgombea wa kiti cha rais nchini Marekani kufadhiliwa na upande wowote kutoka nje ya nchi.
Middle East Eye imeripoti kuwa, matamshi hayo yalichapishwa na shirika rasmi la habari la Jordan, Petra lakini yakafutwa haraka bila ya kutoa maelezo yoyote.
MEE imesema kuwa Saudi Arabia imekuwa na uhusiano wa kifedha na wagombea kiti cha urais nchini Marekani. Vilevile vyombo vya habari vya Marekani vimekuwa vikifichua uhusiano wa kifedha wa Saudi Arabia na familia ya Clinton.