Oct 13, 2025 02:23 UTC
  • Jumatatu, 13 Oktoba, 2025

Leo ni Jumatatu 20 Mfunguo Saba Rabiuthani 1447 Hijria mwafaka na 13 Oktoba 2025 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 2564 iliyopita mji wa kihistoria wa Babel ulitekwa na Kurosh, mwasisi wa utawala wa kizazi cha Hakhamaneshi nchini Iran. Ili kuweza kuudhibiti mji huo ambao ulikuwa na ngome kubwa na imara, Kurosh aliamuru kubadilishwa mkondo wa Mto Tigris uliokuwa ukipita katikati ya mji wa Babel. Kwa utaratibu huo askari wa Kurosh walitumia njia ya zamani ya maji ya mto huo kuingia na kisha kuuteka mji wa Babel. Mji huo ulioko kusini mwa eneo la Mesopotamia katika Iraq ya sasa, ulikuwa katika kilele cha maendeleo na nguvu kubwa katika kipindi hicho.

Kaburi la Kurosh

 

Miaka 312 iliyopita katika siku kama ya leo Haj Lutfali Beig Azar Beigdeli mshairi na mwanafasihi wa Kiirani alizaliwa katika mji wa Isfahan moja ya miji ya Iran. Kipindi Fulani aliishi katika miji ya Qum na Shira Iran. Baada ya kurejea katika safari ya Hija alikata shauri kuishi katika mji aliozaliwa wa Isfahan. Katika kipindi hiki, licha ya njaa na ukosefu wa usalama uliosababishwa na vita nchini Iran, lakini hakuacha kutafuta elimu na alihudhuria masomo ya kundi kubwa la wanazuoni, washairi na watu wenye hekima na kunufaika na kila mmoja wao. Beigdeli alikuwa mahiri katika utunzi wa mashhairi na amevirithisha vizazi viivyokuja baada yake diwani kadhaa za mashairi.

Haj Lutfali Beig Azar Beigdeli

 

Siku kama ya leo miaka 65 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria aliaga dunia Ayatullah Hashim Modarres Qazvini, fakihi na mwanazuoni mahiri wa Iran. Alizaliwa mwaka 1270 HHijria karibu na mji wa Qazvin ulipo magharibi mwa Iran. Hashim Modarres Qazvini alisoma masomo ya msingi ya Fiq'h, Usuul na Falsafa katika mji huuo huuo. Baadaye alielekea katika Chuo Kikuuu cha Kidini cha Isafaha na kubakia huko kwa mud awa miaka 6 na baadaye akahamia katika mji wa Mash'had. Akiwa huko alijishughulisha na kazi ya kufundisha kwa mud awa takribani miaka 40 na kufanikiwa kulea wanafunzi ambao vaadaye waliondokea kuwa wanazuoni mahiri. Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni mmoja wa wanafunzi wa alimu huyu.

Ayatullah Hashim Modarres Qazvini

 

Katika siku kama hii ya leo miaka 61 iliyopita bunge la kimaonyesho la Iran lilipasisha sheria iliyowapa washauri wa kijeshi wa Marekani nchini kinga ya kutofikishwa mahakamani iwapo wangepatikana na hatia ya aina yoyote (Capitulation Accord). Kwa mujibu wa sheria hiyo, wahalifu wa Kimarekani wangehukumiwa nchini kwao kama watatenda jinai nchini Iran, na mahakama za Iran hazikuwa na haki ya kushughulikia kesi zao. Sheria hiyo ilitambuliwa kuwa dharau kwa taifa la Iran na iliyokiuka wazi kujitawala kwa nchi. Kwa msingi huo hayati Imam Ruhullah Khomeini (MA) siku kadhaa baada ya kupasishwa sheria hiyo bungeni alitoa hotuba ya kihistoria akieleza taathira zake na kumshambulia vikali Mfalme Shah na Marekani. Baada ya hotuba hiyo Imam Khomeini alikamatwa na kupelekwa uhamishoni.  ***