Jan 24, 2018 04:34 UTC
  • Jumatano tarehe 24 Januari 2018

Leo ni Jumatano tarehe 6 Jamadil Awwali 1439 Hijria mwafaka na tarehe 24 Januari mwaka 2018.

Siku kama hii ya leo miaka 39 iliyopita sawa na tarehe 4 Bahman mwaka 1357 Hijria Shamsiya, Shapour Bakhtiar Waziri Mkuu wa utawala wa Shah ambaye alikuwa akielewa kuwa kurejea Imam Khomeini nchini kutoka uhamishoni Paris kungempokonya udhibiti wa hali ya mambo, alitoa amri ya kufungwa viwanja vyote vya ndege vya Iran ili kuzuia kurejea nchini Imam Khomeini. Shapour Bakhtiar alichukua hatua hiyo baada ya kuchapishwa habari ya kukaribia kuwasili hapa nchini Imam Khomeini kutoka uhamishoni huko Paris Ufaransa. Hatua hiyo ya serikali ya utawala wa Shah iliwakasirisha wananchi ambao walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa ujio huo wa Imam Ruhullah Khomeini nchini Iran.

Shapour Bakhtiar

Miaka 53 iliyopita katika siku kama ya leo, aliaga dunia Winston Churchill, mwanasiasa maarufu wa Kiingereza akiwa na umri wa miaka 91. Churchill alizaliwa mwaka 1874 na mwaka 1895 alijiunga na jeshi la Uingereza na kushiriki katika vita vya kikoloni. Mwaka 1900 Winston Churchil aliingia katika Bunge la Uingereza akikiwakilisha chama cha Kihafidhina na mara kadhaa aliongoza wizara mbalimbali na kwa vipindi viwili alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.

Winston Churchill,

Katika siku kama ya leo miaka 159 iliyopita, kisima cha kwanza kabisa cha mafuta katika historia kilichimbwa huko Pennsylvania nchini Marekani. Kisima hicho kilichimbwa na Edwin Laurentine Drake kikiwa na kina cha urefu wa mita 230. Uchimbaji wa kisima hicho uliendelea kwa kipindi cha mwaka mmoja. Vifaa vilivyotumika kuchimbia kisima hicho vimehifadhiwa hadi leo katika jumba moja la makumbusho nchini Marekani.

Kisima cha kwanza cha mafuta duniani

Siku kama ya leo miaka 351 iliyopita, mkataba wa Breda ulitiwa saini kati ya Uingereza na Uholanzi. Kwa mujibu wa mkataba huo, Uholanzi ambayo haikuwa na uwezo wa kulinda makoloni yake katika bara lililokuwa ndio kwanza limegunduliwa la Amerika, iliyakabidhi makoaloni yake hayo kwa Uingereza. Eneo muhimu ambalo Uingereza ilikabidhiwa ni New York, ambalo leo kijiografia linapatikana mashariki mwa Marekani.

Mkataba wa Breda baina ya Uingereza na Uholanzi

Na katika siku kama ya leo miaka 1025 iliyopita kwa mujibu wa kalenda ya Hijria aliaga dunia mwanahisabati mashuhuri wa Kiislamu, Abu Said Muhammad bin Abdul Jalil Sistani. Alimu huyo alikuwa amebobea katika nyuga za hisabati, jiometri na nujumu na alihesabiwa kuwa mwalimu mahiri wa taaluma hizo. Abdul Jalil Sistani aliiandika kitabu kuhusiana na kila elimu aliyojifunza na kuwapatia watu wengine ujuzi wake.

 

Tags