Apr 12, 2016 01:30 UTC
  • Jumanne, Aprili 12, 2016

Leo ni Jumanne tarehe 4 Rajab 1437 Hijria sawa na Aprili 12, 2015.

Siku kama ya leo miaka 1279 iliyopita, Zaid bin Ali bin Hussein, mjukuu wa Imam wa Tatu wa Waislamu wa Kishia, alipeperusha bendera ya harakati yake huko mjini Kufa, Iraq wakati wa utawala wa Bani Umayyah. Mapambano ya Zaid ambayo wafuasi wake walitambuliwa kwa jina la Zaidiyyah, yalidumu kwa muda mrefu ambapo mwaka 739 Miladia, aliuawa na Yusuf Ibn Omar Thaqafi, mmoja wa watawala wa Bani Umayyah. Kufuatia matukio hayo, baadhi ya wafuasi wa kiongozi huyo (Zaid bin Ali) ambao hawakuwa Wairani walihamia nchini Yemen na tangu wakati huo Yemen inajulikana kama kituo kikuu cha Waislamu wa Shia Zaidiyyah. Ni bora ikafahamika kuwa, hii leo nusu ya jamii ya Wayemen inaundwa na Mashia Zaidiyyah, Shia Ithna Ashariyyah na Shia Ismailia. Maeneo ambayo wanapatikana zaidi ni kaskazini mwa nchi hiyo.

Siku kama ya leo miaka 96 iliyopita dawa ya kutibu ugonwja wa malaria iligundulika kutoka kwenye magamba ya mti wa Cinchona. Asili ya mti huu wenye majani ya kijani kibichi ni maeneo ya Amerika ya Kusini lakini hii leo unapandwa katika ameneo mengine ya dunia. Utomvu wa mti huu hutumika kutengeneza dawa chungu sana ya Quinine. Tarehe 12 Aprili mwaka 1820 kwa mara ya kwanza kabisa madaktari Pierre Joseph Pelletier na Joseph Bienaimé Caventou wa Ufaransa walifanyika majaribio dawa hiyo ya malaria katika Maabara ya Paris na kukaanza jitihada za kuzalisha dawa ya Quinine.

Siku kama ya leo miaka 55 iliyopita, kwa mara ya kwanza mwanadamu alifika katika anga za mbali na kuizunguka dunia. Siku hiyo Yuri Gagarin mwanaanga wa Urusi ya zamani aliyekuwa na umri wa miaka 27 aliizunguka dunia kwa dakika 89 kwa kutumia chombo cha anga za mbali kwa jina la Vastok 1 na kwa msingi huo kukapatikana mafanikio makubwa katika sekta ya masuala ya anga. Gagarin alifariki dunia akiwa pamoja na mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa sekta ya masuala ya anga wa Urusi ya zamani katika ajali ya ndege hapo mwaka 1968.

Na tarehe 24 Farvardin miaka 8 iliyopita watu kadhaa waliuawa shahidi katika shambulizi la kigaidi lililofanyika katika mji wa Shiraz nchini Iran. Shambulizi hilo lilifanyika kwa bomu lililokuwa limetegwa kwenye kituo cha kidini cha Husainiya ya Mashahiri na kuua watu kadhaa na kujeruhi wengine. Jinai hiyo ilifanywa na vibaraka wa mashirika ya ujasusi ya nchi za kigeni. Baadhi ya vibaraka hao walikamatwa baada ya mlipuko uliotokea katika mojawapo ya hoteli za Tehran na kuadhibiwa kifo baada ya kufikishwa mahakamani.