May 13, 2016 00:05 UTC
  • Ijumaa, Mei 13, 2016

Leo ni Ijumaa tarehe 6 Shaaban 1437 Hijria sawa na 13 Mei 2016.


Miaka 109 iliyopita na katika siku kama ya leo, alizaliwa Bi Daphne du Maurier mwandishi wa riwaya, wasifu na thamthiliya wa Kiingereza. Maurier alizaliwa katika familia ya wanasanaa na iliyokuwa pia na wanafasihi. Ni kutokana na kukulia katika mazingira kama hayo, ndipo Bi Daphne du Maurier alipokuza taratibu kipaji chake katika uwanja wa uandishi. Baada ya kukamilisha masomo yake alielekea Ufaransa. Miongoni mwa vitabu vyake mashuhuri ni Scapegoat au kisingizio na kingine kinaitwa Rebecca. Mwandika wasifu huyo aliaga dunia mwaka 1889.


Siku kama ya leo miaka 303 iliyopita alizaliwa mjini Paris, Alexis Cloude Clairaut mwanahesabati mashuhuri wa Ufaransa. Alikuwa na hamu kubwa na somo la hesabati ambapo akiwa na umri mdogo wa miaka 18 alifanikiwa kujiunga na Chuo cha Sayansi cha Ufaransa. Clairaut alipata umashuhuri mkubwa duniani kutokana na utafiti makini aliofanya katika nyanya tofauti za sayansi. Msomi huyo aliaga dunia mwaka 1765.


Na miaka 125 iliyopita mwafaka na siku hii ya leo, Mirza Hassan Shirazi mmoja wa wasomi wakubwa na marajii wa Kiislamu alitoa fatuwa ya kuharamisha tumbaku nchini Iran kwa shabaha ya kukabiliana na uporaji uliokwua ukifanywa na wakoloni wa kiingereza hapa nchini.  Alizaliwa mwaka 1230 Hijiria katika mji wa Shiraz kusini mwa Iran. Mirza Hassan shirazi aliyetoa fatuwa ya uharamu wa tumbaku na matumizi mengine ya uvutaji wa sigara, fatwa ambayo ilikuwa na lengo la kuzuia malengo ya ukoloni wa Waingereza nchini Iran.