Jun 28, 2016 04:02 UTC
  • Afisa wa zamani wa polisi CAR atuhumiwa kunyonga raia

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limemtuhumu afisa wa zamani wa polisi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kuwa amewanyonga raia kinyume cha sheria.

Human Rights Watch imetangaza leo kuwa, Robert Yékoua-Ketté ambaye alikuwa mkuu wa zamani wa Idara ya Kupambana na Wezi Wanaotumia Silaha (OCRB) ya polisi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati aliwanyonga zaidi ya raia 18 katika kipindi cha kati ya Aprili 2015 na Machi mwaka huu. Taarifa ya HRW imesema: Ushahidi unaonesha kuwa, Robert Yékoua-Ketté alihusika moja kwa moja katika kunyongwa raia 13 na alipaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mchunguzi wa Human Rights Watch, Lewis Mudge ameitaka serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati chini ya usimamizi wa jamii ya kimataifa, kufanya uchunguzi huru kuhusu tuhuma zinazomkabili Yékoua-Ketté.

Robert Yékoua-Ketté aliondolewa madarakani na serikali ya Rais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati tarehe 8 mwezi huu wa Juni.

Tags