Wakongomani waandamana kulalamikia kuuliwa raia wa Kongo nchini India
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i10747-wakongomani_waandamana_kulalamikia_kuuliwa_raia_wa_kongo_nchini_india
Hali ya wasiwasi imetawala Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya watu kumiminika mitaani kulalamikia kuuawa raia mmoja wa nchi hiyo huko India.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 07, 2016 02:54 UTC
  • Wakongomani waandamana kulalamikia kuuliwa raia wa Kongo nchini India

Hali ya wasiwasi imetawala Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya watu kumiminika mitaani kulalamikia kuuawa raia mmoja wa nchi hiyo huko India.

Duru za kuamini za Kongo zimetangaza kuwa, wananchi wenye hasira wa jijini Kinshasa wamefanya maandamano ya kulaani kuuliwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini India.

Habari zinasema kuwa, mwanamke mmoja raia wa Kongo, siku ya Jumapili aliuliwa na mumewe raia wa India.

Duru za kuaminika zimeongeza kuwa, sababu ya mauaji hayo yaliyofanywa na raia huyo wa India haikuweza kujulikana haraka.

Sehemu kubwa ya masoko na maduka makuu ya Kinshasa yamefungwa kutokana na maandamano hayo ya watu wenye hasira. Polisi wamewekwa kila mahali jijini Kinshasa ili kulinda mali za raia na kuwazuia watu wenye hasira wasije wakashambulia mali za watu wenye asili ya India kama njia ya kulipiza kisasi.