Waislamu wa Tanzania wamkumbuka na kumuenzi Sayyid Hassan Nasrullah
(last modified Thu, 14 Nov 2024 11:27:55 GMT )
Nov 14, 2024 11:27 UTC
  • Waislamu wa Tanzania wamkumbuka na kumuenzi Sayyid Hassan Nasrullah

Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania wamefanya kumbukumbu ya Arubaini ya Sayyid Hassan Nasrullah aliyekuwa Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.

Kumbukumbu hiyo imefanyika mjini Dar es Salaam katika Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuhudhuriwa na shakhsia mbalimbali wa kidini.

Viongozi wengi wa dini, balozi wa Iran nchini Tanzania, wanafunzi wa vituo mbalimbali vya Kiislamu, jumuiya za Lebanon, Syria na India walishiriki katika shughuli hiyo.

Katika kumbukumbu hiyo ya Arubaini ya shahidi Sayyid Nasrullah  mbali na kuenziwa mashahidi wa muqawama kulikusanywa pia misaada ya watu kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Gaza na Lebanon.

Aidha kuliandaliwa ratiba mbalimbali kwa ajili ya kuwafahamisha watu jinai za utawala wa Kizayuni na ukandamizaji unaofanywa na utawala huo ghasibu dhidi ya wananchi wasio na hatia wa  Palestina na Lebanon.

Ikumbumbwe kuwa, Septemba 27, utawala wa kigaidi wa Israel ulimuua shahidi Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyidd Hassan Nasrullah katika shambulio la kinyama lililolenga eneo la Adh-Dhaahiya Kusini, lililoko kwenye viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo, Beirut.