Chad yakata uhusiano wa kijeshi na Ufaransa
Chad imehitimisha makubaliano iliyofikia na Ufaransa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika nyanja za usalama na ulinzi kati ya nchi mbili.
Taarifa ya jana ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Chad imeeleza kuwa serikali ya Jamhuri ya Chad inabainisha kuhusu maoni ya kitaifa na kimataifa kuhusu uamuzi wake wa kusitisha mkataba wa ushirikiano wa kiulinzi uliousaini na Ufaransa.
Taarifa hiyo ambayo imesainiwa na Abderaman Koulamallah Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad imeeleza kuwa baada ya miongo kadhaa ya uhuru wa nchi hiyo; wakati umefika sasa kwa Chad kuwa na mamlaka kamili na kutazama upya ushirikiano wake wa kimkakati kwa mujibu wa maslahi ya taifa."
Uamuzi huu tajwa ulitangazwa juzi Jumatano wakati wa ziara ya Waziri wa Ufaransa wa Mambo ya Nje na masuala ya Ulaya Jean-Noel Barrot huko Chad.
Itakumbukwa kuwa uongozi wa kijeshi wa Mali pia mwaka 2022 ulitangaza uamuzi sawa na huu wa Chad wa kusitisha ushirikiano wa kijeshi na Ufaransa.