Afrika Kusini: Tunaendelea kushikamana na wananchi wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i122464-afrika_kusini_tunaendelea_kushikamana_na_wananchi_wa_palestina
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa nchi hiyo itaendelea kushikakama na kuwa pamoja na wananchi wa Palestina.
(last modified 2025-02-08T04:25:14+00:00 )
Feb 08, 2025 04:25 UTC
  • Afrika Kusini: Tunaendelea kushikamana na wananchi wa Palestina

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa nchi hiyo itaendelea kushikakama na kuwa pamoja na wananchi wa Palestina.

Rais wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa nchi hiyo itaendelea kuwa pamoja na bega kwa bega na wananchi madhulumu wa Palestina. Amesema Wapalestina kwa miongo kadhaa sasa wamevumilia mateso chini ya uvamizi haramu wa utawala wa Kizayuni.

Rais Cyril Ramaphosa ameongeza kuwa: Afrika Kusini imewasilisha mashtaka dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa kuzingatia wajibu wake chini ya Mkataba wa Kuzuia Mauaji ya Kimbari.

Afrika Kusini Disemba mwaka juzi iliwasilisha mashtaka katika mahakama hiyo dhidi ya utawala wa Kizayuni na kutangaza kuwa utawala huo umekiuka mkataba unaozuia mauaji ya kimbari mkabala wa raia wa Palestina wa Ukanda wa Gaza. 

Nchi kadhaa zikiwemo Nicaragua, Cuba, Ireland, Colombia, Libya, Mexico, Palestina, Uhispania na Uturuki zimejiunga na  Afrika Kusini katika mashtaka hayo dhidi ya Israel. 

Katika upande mwingine, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya mjini Hague Uholanzi siku ya Alhamisi, tarehe 21 Novemba mwaka jana ilitoa waranti ya kukamatwa  Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, na Yoav Galant, Waziri wa Vita wa zamani wa utawala huo kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita, jinai dhidi ya ubinadamu, na kuwasababishia njaa Wapalestina kama silaha ya kivita.