Serikali ya Uganda yakanusha tuhuma za kutenda mauaji ya kiholela
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i20443-serikali_ya_uganda_yakanusha_tuhuma_za_kutenda_mauaji_ya_kiholela
Serikali ya Uganda imekanusha tuhuza dhidi yake kwamba imefanya mauaji ya kiholela nchini humo.
(last modified 2025-11-19T08:00:07+00:00 )
Nov 30, 2016 03:18 UTC
  • Serikali ya Uganda yakanusha tuhuma za kutenda mauaji ya kiholela

Serikali ya Uganda imekanusha tuhuza dhidi yake kwamba imefanya mauaji ya kiholela nchini humo.

Jeje Odongo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uganda  jana alikanusha tuhuma zilizowasilishwa kwa serikali na Amnesty Internatinal kuwa imefanya mauaji ya kiholela nchini humo na kueleza kuwa, askari usalama walilazimika kujilinda baada ya kushambuliwa na wale waliowataja kuwa ni waasi. Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International limewatuhumu askari usalama wa Uganda kuwa wametekeleza mauaji ya kiholela wakati yalipojiri mapigano hivi karibuni katika eneo moja lakikabila nchini humo. Abdullahi Halakhe Afisa wa Amnesty International katika Kanda ya Afrika Mashariki amesema kuwa picha ya mauaji hayo haijawekwa wazi na kwamba ukatili huo ni wa kutisha na uliokiuka haki za binadamu.

Maafisa wa Uganda wamedai kuwa walinzi 46 na polisi 16 wameuawa katika shambulio lililofanywa na askari usalama wa nchi hiyo katiak ikulu ya Charles Wesley Mumbere Mfalme wa Rwenzururu ambaye anatuhumiwa kuwaongoza waasi Amnesty International imeeleza kuwa askari usalama wa Uganda walifyatua risasi bila ya kuchukua tahadhari na hatimaye kuwauwa raia wengi kiholela. 

Charles Wesley Mumbere Mfalme wa Rwenzururu

Shirika hilo limeeleza kuwa wapiganaji 46 wanaounga mkono mfumo wa kifalme nchini Uganda na maafisa 16 wa polisi waliuawa katika mapigano hayo yaliyotokea mwishoni mwa wiki katika mji wa Kasese katika mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.