Feb 15, 2017 15:47 UTC
  • ECCAS yatoa wito wa kukomeshwa machafuko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Katikati mwa Afrika ECCAS imesisitiza kuwa, kuna haja ya kukomeshwa machafuko katika Jamhutri ya Afrika ya Kati.

Taarifa ya Jumuiya ya ECCAS imezitaka pande zinazozozana katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) zisitishe mapigano na hivyo kuandaa mazingira ya kurejeshwa amani na utulivu katika nchi hiyo.

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Katikati mwa Afrika sambamba na kuonyesha wasiwasi mkubwa ilio nao kutokana na hali mbaya ya ukosefu wa amani na usalama katika nchi hiyo imevitaka vikosi vya Chama cha Wananchi Kwa Ajili ya Mwamko Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (FPRC) na Muungano Kwa Ajili ya Amani (UPC) kuvumiliana na kusitisha haraka uhasama baina yao.

Askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa CAR

Aidha sehemu nyingine ya taarifa ya ECCAS imezitaka pande hizo zinazopigana huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kuchagua njia za amani kwa ajili ya kutatua mizozo na hitilafu baina yao kupitia mipango ya Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kiuchuni ya nchi za Katikati mwa Afrika.

Mapigano kati ya Chama cha Wananchi Kwa Ajili ya Mwamko Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (FPRC) na Muungano Kwa Ajili ya Amani (UPC) yamekuwa yakishuhudiwa nchini humo tangu Novemba mwaka jana. Mapigano hayo yamezidi kuvuruga usalama wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo imekuwa ikishuhudia machafuko kwa muda sasa. 

Tags