Spika Zuberi: Mazungumzo yanaweza kutatua mgogoro Zanzibar, hakuna uchaguzi hadi 2020
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25760-spika_zuberi_mazungumzo_yanaweza_kutatua_mgogoro_zanzibar_hakuna_uchaguzi_hadi_2020
Hivi karibuni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alikuwa safarini nchini Iran na Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran ilizungumza naye kuhusu mgogoro wa kisiasa unaeondelea Zanzibar.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Feb 28, 2017 13:45 UTC

Hivi karibuni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alikuwa safarini nchini Iran na Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran ilizungumza naye kuhusu mgogoro wa kisiasa unaeondelea Zanzibar.

Mgogoro huo uliibuka baada ya chama cha upinzani CUF kususia uchaguzi  wa rais uliorudiwa Machi 2016 na kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi huo uliopelekea kuchaguliwa Rais Dkt. Ali Mohamed Shein kuendelea kuongoza Zanzibar. Chama cha CUF kilikataa kutambua uchaguzi huo huku kikipinga hatua ya Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar ZEC kubatilisha uchaguzi wa Rais  uliofanyika Oktoba 2015.

Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa Radio Tehran, Mubarak  Henia, Mheshimiwa Zuberi  amesema kuna uwezekano wa mgogoro wa uliopo Zanzibar kutatuliwa kwa mazungumzo lakini akasisitiza kuwa hakuna uchaguzi mpya utakaofanyika hadi mwaka 2020.