Mar 08, 2016 07:35 UTC
  • Watu wawili wauawa katika machafuko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Watu wawili wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika machafuko yaliyotokea kwenye eneo la Durba mkoani Haut Uélé kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ripoti kutoka mkoani Haut Uélé zinaeleza kuwa machafuko na mapigano yalizuka wakati vijana kadhaa wanachama wa muungano wa vijana wa eneo la Durba walipokuwa wakiandamana wakidai kupatiwa maeneo ya uchimbaji madini ya dhahabu kama walivyokuwa wameahidiwa na viongozi wa serikali.

Odon Buleri, mkuu ya asasi ya kiraia katika eneo la Durba amesema kabla ya uingiliaji kati wa polisi kwa lengo la kuawatawanya waandamanaji, maandamano hayo yalikuwa yakiendelea katika mazingira ya amani. Kwa mujibu wa Buleri, awali vikosi vya polisi na jeshi la serikali vilifyatua risasi hewani na hatimaye kuwalenga waandamanaji na kusababisha vijana wawili kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Waandamanaji nao waliwashambulia askari kwa mawe kujibu ufyatuaji riasi huo uliofanywa dhidi yao.../

Tags