Kiongozi wa zamani wa Ikhwanul Muslimin aaga dunia katika jela ya Misri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31230-kiongozi_wa_zamani_wa_ikhwanul_muslimin_aaga_dunia_katika_jela_ya_misri
Mwakilishi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri (Muslim Brotherhood) ametangaza kuwa kiongozi wa zamani wa harakati hiyo, Mohammed Mahdi Akef ameaga dunia akiwa katika jela ya utawala wa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jul 02, 2017 03:28 UTC
  • Kiongozi wa zamani wa Ikhwanul Muslimin aaga dunia katika jela ya Misri

Mwakilishi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri (Muslim Brotherhood) ametangaza kuwa kiongozi wa zamani wa harakati hiyo, Mohammed Mahdi Akef ameaga dunia akiwa katika jela ya utawala wa nchi hiyo.

Muntasir al-Zayyat amethibitisha kuwa Mohammed Mahdi Akef, kiongozi wa zamani wa Ikhwanul Muslimin amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 katika jela ya serikali ya Cairo alikokuwa akitumikia kifungo.

Akef alishika hatamu za uongozi wa harakati hiyo kubwa zaidi ya kisiasa ya Misri mwaka 2014 baada ya kufariki dunia Maamun al Hudhaibi na alikabidhi uongozi wa chama kwa Muhammad Badie.

Wanachama wengi wa Ikhwanul Muslimina wanashikiliwa jela, Misri

Tangu ilipoingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi, serikali ya Jenerali mstaafu, Abdul Fattah al Sisi imekuwa ikitekeleza siasa za kukandamiza harakati zote za upinzani hususan chama cha Ikhwanul Muslimin (Muslim Brotherhood) na aghlabu ya viongozi wa chama hicho wamehukumiwa vifo au vifungo jela. 

Mohammed Mahdi Akef alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2013.