Ufaransa yasisitiza kupambana na ugaidi barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31242-ufaransa_yasisitiza_kupambana_na_ugaidi_barani_afrika
Rais wa Ufaransa amesisitizia udharura wa kupambana ugaidibarani Afrika. Amesisitiza hayo leo katika kikao kilichofanyika Bamako, mji mkuu wa Mali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 02, 2017 10:31 UTC
  • Rais Emanuel Macron wa Ufaransa
    Rais Emanuel Macron wa Ufaransa

Rais wa Ufaransa amesisitizia udharura wa kupambana ugaidibarani Afrika. Amesisitiza hayo leo katika kikao kilichofanyika Bamako, mji mkuu wa Mali.

Rais Emanuel Macron wa Ufaransa aidha amesisitizia wajibu wa kuangamizwa makundi ya kigaidi barani Afrika na kusema kuwa: Ufaransa na nchi nyingine washirika wake barani Afrika zinapaswa kuendesha mapambano endelevu dhidi ya magaidi katika eneo la Sahel barani humo.   

Amesema, Ufaransa inatilia mkazo suala la kutoa misaada ya kilojistiki kwa ajili ya oparesheni za pamoja za wanajeshi wa eneo la Sahel barani Afrika na za vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vinavyoendesha mapambano dhidi ya ugaidi katika eneo hilo.  

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na wa Ufaransa wako nchini Mali tangu katikati ya mwaka 2013, hata hivyo vikosi hivyo vimeshindwa kurejesha amani ya kudumu nchini humo huku vitisho vya kigaidi vikiendelea kuwepo.

Wanajeshi wa Ufaransa wakipiga doria nchini Mali  

Eneo la Sahel la Afrika linaanzia magharibi hadi mashariki mwa bara hilo, na kuendelea hadi kaskazini mwa Senegal, kusuini mwa Mauritania, katikati mwa Mali, kusini mwa Algeria na Niger, katikati mwa Chad, Kusini mwa Sudan, Kaskazini mwa Sudan na kusini mwa Eritrea.