Makumi wauawa katika shambulio la kigaidi Sinai, Misri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31456-makumi_wauawa_katika_shambulio_la_kigaidi_sinai_misri
Wanajeshi wasiopungua kumi wameuawa katika shambulio la kigaidi lililofanyika leo huko Sinai kaskazini mwa Misri.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jul 07, 2017 10:48 UTC
  • Makumi wauawa katika shambulio la kigaidi Sinai, Misri

Wanajeshi wasiopungua kumi wameuawa katika shambulio la kigaidi lililofanyika leo huko Sinai kaskazini mwa Misri.

Jeshi la Misri limetangaza kuwa, wanajeshi 23 wameuawa baada ya gari lililokuwa limetegwa bomu kulipuka katika kituo cha upekuzi cha jeshi katika Peninsula ya Sinai huko kaskazini mwa nchi hiyo. Wanajeshi wengine 33 wamejeruhiwa katika shambulio hilo. 

Akari jeshi wa Misri akiwa katika doria katika kituo cha upekuzi cha Sinai baada ya kujiri shambulizo la kigaidi 

Baada ya shambulizi hilo wanajeshi wa Misri walifyatua risasi na kupambana na magaidi walioshambulia kituo hicho cha upekuzi  na kufanikiwa kuwaangamiza 40 miongoni mwao. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na hujuma hiyo.

MKoa wa Sinai ya kaskazini huko Misri ni moja ya ngome kuu za tawi la wanamgambo wenye mfungamano na kundi la kigaidi la Daesh ambalo linaendesha harakati zake katika eneo hilo.