Ripoti: Serikali ya Misri imeua raia 135 kinyume cha sheria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i32826-ripoti_serikali_ya_misri_imeua_raia_135_kinyume_cha_sheria
Taasisi ya Kuratibu Masuala ya Haki za Binadamu na Uhuru nchini Misri imefichua kwamba, karibu watu 135 wameuawa kinyume cha sheria nchini humo katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu wa 2017.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 07, 2017 12:04 UTC
  • Ripoti: Serikali ya Misri imeua raia 135 kinyume cha sheria

Taasisi ya Kuratibu Masuala ya Haki za Binadamu na Uhuru nchini Misri imefichua kwamba, karibu watu 135 wameuawa kinyume cha sheria nchini humo katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu wa 2017.

Gazeti la al Quds al Arabi linalochapishwa London nchini Uingereza limeripoti kuwa, Taasisi ya Kuratibu Masuala ya Haki za Binadamu na Uhuru nchini Misri imefichua kuwa, kesi 90 za mateso ya wafungwa wa kisiasa na kutelekezwa mahabusi wagonjwa bila ya kupewa huduma za tiba zimesajiliwa katika jela na korokoro mbalimbali za Misri.

Ripoti ya taasisi hiyo ya kutetea haki za binadamu imesema kuwa, mashambulizi na mateso ya askari usalama wa Misri dhidi ya raia pia limekuwa jambo la kawaida. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu wa 2017 kumesajiliwa kesi za kutoweka wanaume 254 na kwamba 47 kati yao tu ndio waliopatikana. 

Mahabusu wanateswa na kunyanyaswa Misri

Serikali ya Misri imekuwa ikiwakandamiza wanaharakati wa kisiasa na wafuasi wa vyama vya upinzani kwa kisingizio cha kupambana na magenge ya kigaidi. Cairo pia imepiga marufuku shughuli zote za kisiasa za chama kikuu cha upinzani cha Ikhwanul Muslimin