Nchi za Afrika zaendelea kuunga mkono azimio la UN kuhusu Quds
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i37987-nchi_za_afrika_zaendelea_kuunga_mkono_azimio_la_un_kuhusu_quds
Nchi na jumuiya mbalimbali za Kiafrika zimeendelea kuunga mkono azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililopinga hatua ya Marekani ya kuitambua Quds tukufu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 23, 2017 15:25 UTC
  • Nchi za Afrika zaendelea kuunga mkono azimio la UN kuhusu Quds

Nchi na jumuiya mbalimbali za Kiafrika zimeendelea kuunga mkono azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililopinga hatua ya Marekani ya kuitambua Quds tukufu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala haramu wa Israel.

Hatua hiyo ya nchi za Afrika imechukuliwa kufuatia hatua ya Alkhamisi iliyopita ambapo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipasisha muswada uliopendekezwa na Misri unaolaani na kupinga uamuzi wa Marekani wa kutambua rasmi Quds kuwa ni mji mkuu wa Israel. Nchi za Afrika zimechukua msimamo huo licha ya Rais Donald Trump wa Marekani kutishia kwamba, atakata misaada ya kifedha kwa nchi yoyote itakayounga mkono azimio hilo.

Togo ilikuwa nchi peke ya Afrika iliyopinga azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Marekani ilipingwa hata na waitifaki wake katika Baraza Kuu la UN

Wizara ya Mambo ya Nje ya Botswana imejibu vitisho vya Marekani kwa kutoa taarifa iliyosisitiza kuwa, Gaborone haitatishwa na vitisho hivyo na itatoa kura yake kwa kufuata haki ya kujitawala na misingi ya siasa zake za kigeni. 

Serikali ya Uganda pia imetoa taarifa ikiitaja Marekani kuwa ni nchi ya kijuba na kibabe. 

Jamii ya Waislamu wa Zambia pia imeunga mkono azimio la UN na kupinga matakwa na viatisho vya Marekani.