Watu 50 wauawa katika mapigano ya kikabila kaskazini mwa Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i38455-watu_50_wauawa_katika_mapigano_ya_kikabila_kaskazini_mwa_nigeria
Watu wasiopungua 50 wameuawa kaskazini mwa Nigeria na makumi ya wengine klujeruhiwa kufuatia mapigano ya kikabila yaliyozuka baina ya makabila mawili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 03, 2018 00:54 UTC
  • Watu 50 wauawa katika mapigano ya kikabila kaskazini mwa Nigeria

Watu wasiopungua 50 wameuawa kaskazini mwa Nigeria na makumi ya wengine klujeruhiwa kufuatia mapigano ya kikabila yaliyozuka baina ya makabila mawili.

Gavana wa jimbo la Benue amewaambia waandishi wa habari kwamba, mapigano hayo yalitokea jana baada yakabila la Fulani kushambulia eneo la Tse moja ya vitongoji vya jimbo hilo na kupelekea kuibuka mapigano kati ya pande mbili.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, wafanya shambulio hilo walikuwa wafugaji wa kabila la Fulani waliowashambulia wakulima wa Tse kaskazini mwa Nigeria.

Miongoni mwa waliouawa ni wanawake na watoto wadogo huku baadhi ya majeruhi hali zao zikiripotiwa kuwa mbaya.

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria

Gavana wa jimbo la Benue ameikosoa serikali kuu ya Nigeria akisema kwamba, ilitahadharishwa kuhusiana na vitisho vya mara kwa mara vya wagujai wa kabila la Fulani.

Inaelezwa kuwa, kutokana na ukame unaoikumba Nigeria watu wa kabila la Fulani wanakabiliwa na umasikini na kila mara wamekuwa wakiwashambulia wakulima wa makabila mengine na kupora mali na mifugo yao.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria yanakabiliwa na ukosefu wa amani kutokana na mashambulio ya wanamgambo wa kundi la kkigaidi la Boko Haram.