Watu wenye silaha waua watu 27 kaskazini mwa Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i43418-watu_wenye_silaha_waua_watu_27_kaskazini_mwa_nigeria
Maafisa wa serikali ya Nigeria wametangaza habari ya kuuawa watu 27 katika mashambulizi ya magenge yenye silaha kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 21, 2018 02:47 UTC
  • Watu wenye silaha waua watu 27 kaskazini mwa Nigeria

Maafisa wa serikali ya Nigeria wametangaza habari ya kuuawa watu 27 katika mashambulizi ya magenge yenye silaha kaskazini mwa nchi hiyo.

Maafisa hao wamesema kuwa, makundi yenye silaha yalifanya mashambulizi jana Ijumaa kaskazini mwa Nigeria na kuua watu wasiopungua 27.

Lawwali Usmanu, mmoja wa wakazi wa eneo la Kabaro huko kaskazini mwa Nigeria amesema, watu 20 wameuawa katika shambulio lililofanywa kwenye eneo hilo na wengine saba wameuwa katika eneo la Danmami huko huko kaskazini mwa Nigeria.

Wanajeshi wa Nigeria katika kampeni za kupambana na magenge yenye silaha

 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, siku ya Alkhamisi majambazi walifanya mashambulizi katika vijiji viwili vya jimbo la Zamfara, kaskazini mwa Nigeria kwa lengo la kuiba mifugo. Wanajeshi wa serikali wametumwa katika eneo hilo kukabiliana na wahalifu hao.

Hivi sasa mashambulizi ya watu wenye silaha na wizi wa mifugo umeongezeka sana katika maeneo ya kaskazini mwa Nigeria.

Maafisa wa serikali ya nchi hiyo wamesema kuwa, wezi wa mifugo wameshaua watu 26 katika eneo la Anka katika nusu ya pili ya mwezi huu wa Aprili, huko kaskazini mwa Nigeria.