Apr 04, 2016 16:35 UTC
  • Polisi ya Congo yapambana na waasi wa Ninja

Milio ya risasi imesikika mapema leo katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, Brazaville na watu walioshuhudia wanasema kuwa polisi ya nchi hiyo inapambana na kundi la waasi wa "Ninja".

Afisa wa serikali ya Brazaville ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa, polisi ya nchi hiyo inapambana na waasi wa kundi linalojiita "Ninja" na kwamba maafisa wa serikali wanadhibiti hali ya mambo.

Mapigano baina ya serikali ya Congo na kundi la Ninja ambalo linataka kushirikishwa zaidi katika serikali yalianza miaka mingi iliyopita. Kundi hilo lilikuwa miongoni mwa makundi ya upinzani katika vita vya ndani vya 1998 hadi 1999 na lilitia saini makubaliano ya amani na serikali mwaka 2003.

Mapigayo ya leo yametokeo wiki kadhaa baada ya Denis Sassou Nguesso kushinda tena kiti cha rais wa nchi hiyo kwa kupata asilimia 60 ya kura zilizopigwa.

Mapigano hayo yamezusha wasiwasi kiasi kwamba Ufaransa, muitifaki mkubwa wa Congo Brazaville, imewatahadharisha raia wake walioko nchini humo na kuwataka wabakie majumbani mwao.

Tags