May 13, 2018 15:45 UTC
  • Kongo DR na UN zatuma wataalamu kukabiliana na mlipuko wa Ebola

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na taasisi za Umoja wa Mataifa zimeanza kutuma nchini humo timu za wataalamu ili kujaribu kuzuia kuenea maambukizi ya homa ya Ebola ambayo hadi sasa inashukiwa tayari imeshawaambukiza watu zaidi ya 30.

Kesi ya mtu mmoja anayesadikiwa kuambukizwa homa ya Ebola iliripotiwa Ijumaa iliyopita katika mkoa wa Equateur kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao Waziri wa Afya wa  nchi hiyo Oly Ilunga Kalenga aliuzuru hapo jana akiwa pamoja na maafisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa umoja huo (UNICEF).  Baada ya kuutembelea mkoa huo wa Equateur, Waziri wa Afya wa Kongo ameeleza kuwa na hapa ninamnukuu" tunapaswa kufanya juhudi haraka iwezekanavyo na kushirikiana na serikali ili kupambana ipasavyo na mlipuko huo mpya wa maambukizi," mwisho wa kunukuu.

Mkoa wa Equateur nchini Kongo uliokumbwa na maambukizo ya Ebola  

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  Jumanne iliyopita kwa mara ya kwanza iliripoti mlipuko huo wa homa ya Ebola katika kijiji cha Ikoko Impenge karibu na mji wa Bikoro; huku watu 32 wakishukiwa kuugua homa hiyo pamoja na watu wengine 18 wakiripotiwa kuaga dunia tangu Aprili 4 mwaka huu. Maafisa husika wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanafanya kila wawezalo kuhakikisha virusi vya homa ya Ebola havisambai na kushindwa kudhibitiwa kama ilivyotokea huko magharibi mwa Afrika kati ya mwaka 2014 hadi 2016 na kuuwa watu zaidi ya 11,300 katika nchi za Guinea Conakry, Sierra Leone na Liberia. 

 

 

 

 

 

Tags