Wahajiri haramu 35 wafariki baada ya boti yao kuzama baharini Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i45358-wahajiri_haramu_35_wafariki_baada_ya_boti_yao_kuzama_baharini_tunisia
Wahajiri 35 haramu wamepoteza maisha baada boti yao kuzama baharini nchini Tunisia huku wengine 67 wakiokolewa katika oparesheni ya gadi ya pwani ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 03, 2018 10:28 UTC
  • Wahajiri haramu 35 wafariki baada ya boti yao kuzama baharini Tunisia

Wahajiri 35 haramu wamepoteza maisha baada boti yao kuzama baharini nchini Tunisia huku wengine 67 wakiokolewa katika oparesheni ya gadi ya pwani ya nchi hiyo.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Tunisia imesema miongoni mwa wahajiri hao kulikuwa na raia wa kigeni na pia raia wa Tunisia. Maafisa wa usalama wanasema boti iliyozama ilikuwa na wahajiri 180, wakiwemo raia 80 kutoka nchi zingine za Afrika waliokuwa wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterania kuelekea Ulaya.

Magenge ya kuwasafirisha wanadamu sasa yanatumia Tunisia kuwavukisha wahajiri wanaoelekea  Ulaya baada ya gadi ya pwani ya Libya kuimarisha usalama na kufanikiwa kuzuia magenge yaliyokuwa yakitumia pwani ya nchi hiyo.

Wahajiri haramu wakiokolewa

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhajiri IOM, zaidi ya wakimbizi elfu tatu waliaga dunia mwaka jana wakijaribu kufika Ulaya kupitia Bahari ya Mediterania, akthari ya wahajiri hao wakiwa ni raia wa nchi za Kiafrika ambao wanataraji kupata maisha mazuri na ajira huko barani Ulaya kutokana na masaibu katika nchi zao.

Zaidi ya watu 87,000 walihatarisha maisha yao katika safari hizo za baharini za kuogofya, wakijaribu kufika Yemen mwaka jana pekee.