EU yaishambulia Imarati kwa kuvuruga uthabiti Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46602-eu_yaishambulia_imarati_kwa_kuvuruga_uthabiti_somalia
Bunge la Umoja wa Ulaya limezikosoa vikali Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia kwa kuikatia Somalia misaada kutokana na nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kutangaza msimamo wa kutoegemea upande wowote katika mgogoro kati ya nchi nne za Kiarabu zikiongozwa na Saudia kwa upande mmoja na Qatar kwa upande wa pili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 06, 2018 08:57 UTC
  • EU yaishambulia Imarati kwa kuvuruga uthabiti Somalia

Bunge la Umoja wa Ulaya limezikosoa vikali Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia kwa kuikatia Somalia misaada kutokana na nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kutangaza msimamo wa kutoegemea upande wowote katika mgogoro kati ya nchi nne za Kiarabu zikiongozwa na Saudia kwa upande mmoja na Qatar kwa upande wa pili.

Taarifa ya Bunge la EU lenye makao yao nchini Ubelgiji imetoa mwito wa kusitishwa hatua zozote zinazoweza kuyumbisha uthabiti wa Somalia, sawa na kuheshimiwa maamuzi na uhuru wa kujitawala nchi hiyo ya Kiafrika.

Hii ni katika hali ambayo, Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani katika mazungumzo yake na Rais Mohammad Abdullahi Farmajo wa Somalia hivi karibuni aliahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Somalia za kurejesha uthabiti na uhuru wa kujitawala, kama ambavyo aliahidi kuendelea kuifadhili nchi hiyo inayokabiliwa na migogoro mbalimbali.

Itakumbukwa kuwa,  mwezi Aprili mwaka huu serikali ya Abu Dhabi ilichukua hatua ya kufunga hospitali yake mjini Mogadishu, wiki moja baada ya serikali ya Somalia kutangaza kusitisha shughuli za Imarati kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo, ikiwa ni baada ya kutaifisha dola milioni 10 za Abu Dhabi katika uwanja wa ndege wa Mogadishu.

Saudia na waitifaki wake imeiweka Qatar chini ya mzingiro wa kila upande

Mivutano kati ya Somalia na Imarati ilishtadi kufuatia kuzorota uhusiano kati ya Qatar na nchi nne za Kiarabu, yaani Saudia, Misri, Imarati na Bahrain ambapo Somalia ilitangaza kutokuwa upande wowote katika mgogoro huo.

Hii ni katika hali ambayo, Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia amewahi kuonya kwamba, serikali na wananchi wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika wanapinga uingiliaji wa madola ya kigeni katika masuala ya ndani ya nchi hiyo