Waziri Mkuu wa Madagascar amejiuzulu pamoja na baraza lake la mawaziri.
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i4681-waziri_mkuu_wa_madagascar_amejiuzulu_pamoja_na_baraza_lake_la_mawaziri.
Taarifa ya kujiuzulu Jean Ravelonarivo Waziri Mkuu wa Madagascar na baraza lake la mawaziri ilitolewa jana Ijumaa na afisa katika ofisi ya rais ambaye hakutoa maelezo yoyote.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 08, 2016 23:26 UTC
  • Waziri Mkuu wa Madagascar amejiuzulu pamoja na baraza lake la mawaziri.

Taarifa ya kujiuzulu Jean Ravelonarivo Waziri Mkuu wa Madagascar na baraza lake la mawaziri ilitolewa jana Ijumaa na afisa katika ofisi ya rais ambaye hakutoa maelezo yoyote.

Roger Ralala Katibu Mkuu katika ofisi ya Rais wa Madagascar amesema kuwa Rais amepokea hatua ya kujiuzulu Waziri Mkuu na mawaziri wote wa serikali. Ravelonarivo aliingia madarakani mwezi Januari mwaka jana, baada ya Madagascar kukumbwa na tatizo la umeme, tatizo la ajira na kuzorota uchumi wa nchi, masuala yaliyoundoa madarakani utawala uliotangulia.

Waziri Mkuu wa Madagascar aliyejizulu jana Ijumaa, mwezi Julai mwaka jana alinusurika kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, baada ya mrengo wa upinzani wa Mapar kuwasilisha hoja bungeni ukisema kuwa hauridhishwi na mwendo wa kinyonya wa hatua za mageuzi za serikali katika kisiwa hicho kinachopatikana katika bahari ya Hindi.