Aug 15, 2018 14:00 UTC
  • Kongo yaanza matibabu ya majaribio kwa homa ya Ebola

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeanza kutumia dawa ya majaribio aina ya mAb114 kutibu mlipuko wa karibuni wa homa hiyo inayosababishwa na virusi.

Hayo yamesemwa na maafisa wa afya wa nchi hiyo. Hii ni mara ya kwanza kwa Kongo kutumia matibabu hayo ya majaribio kukabiliana na kuenea kwa kasi kwa homa hiyo. 

Watu 42 wanaamika kupoteza maisha kutokana na homa hiyo ya kuvuja damu katika milipuko kumi kuwahi kuiathiri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu ilipogunduliwa katika muongo wa 70. Wizara ya Afya ya Kongo imetangaza kuwa hadi kufikia sasa watu 66 wameripotiwa kuambukizwa homa ya ebola huku 39 wakithibitishwa kuugua maradhi hayo.  Mlipuko wa homa ya ebola umeenea kutoka katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini hadi katika mkoa wa jirani wa Ituri baada ya kurejea nyumbani mtu mmoja aliyekuwa amembukizwa. Hatua hiyo imefanya jitihada za kuzuia kuenea homa hiyo hatari kuwa ngumu kwa kuzingatia kuwa eneo hilo kuathiriwa na machafuko ya wanamgambo wenye silaha.  

 

Tags