Sep 13, 2018 13:45 UTC
  • Wafungwa wa kisiasa wanakabiliwa na hali mbaya katika jela za Misri

Hali ya wafungwa wa kisiasa nchini Misri miaka mitano baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo inaripotiwa kuwa mbaya sana.

Anwar Al-Jamawi mtafiti wa Ulimwengu wa Kiarabu ameandika kuwa baada ya kupita miaka 5 tangu baada ya mapinduzi yaliyoiondoa madarakani serikali ya kidemokrasia ya nchi hiyo, Misri inashuhudia ukiukwaji usio na kifani wa haki za binadamu na kwamba serikali ya Cairo inaendeshwa na kundi la watu makhsusi.  

Al-Jamawi ameashiria mapinduzi ya jeshi yaliyoongozwa na Rais wa sasa wa Misri Jenerali Abdul Fattah al Sisi dhidi ya Muhammad Morsi mwezi Julai mwaka 2013 na kusema kuwa, kutokana na mbinyo na ukandamizaji wa uhuru wa kiraia na vyombo vya habari na vile vile ukandamizaji wa wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wanasheria na wanaharakati wa masuala ya kijamii; jela za Misri zimejaa wafungwa wa kisiasa ambao wanashikiliwa kwa tuhuma ambazo hazijathibitishwa. 

Muhammad Morsi, Rais  wa Misri aliyepinduliwa madarakani baada ya kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia 

 

Ripoti za jumuiya ya kutetea haki za binadamu zinaarifu kuwa idadi ya wafungwa wa kisiasa nchini Misri inafikia watu elfu 65. Wafungwa hao wako katika jela 64 tofauti kwa makosa ya kushiriki kwenye maandamano ya amani, kutoa maoni na wengine kwa kosa eti la kujiunga na makundi mbalimbali bila ya ruhusa ya serikali.  

Ripoti iliyotolewa na kituo cha uratibu wa masuala ya haki za binadamu nchini Misri inasema kuwa watu 439 wamefariki dunia katika jela za nchi hiyo tangu tarehe 3 Julai mwaka 2013.

 

Tags