Al Burhan: Kumefanyika majaribio kadhaa ya mapinduzi Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i54631-al_burhan_kumefanyika_majaribio_kadhaa_ya_mapinduzi_sudan
Mkuu wa Baraza la Kijeshi linalotawala Sudan amesema kuwa jeshi la nchi hiyo imezima majaribio kadhaa ya mapinduzi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 08, 2019 06:26 UTC
  • Al Burhan: Kumefanyika majaribio kadhaa ya mapinduzi Sudan

Mkuu wa Baraza la Kijeshi linalotawala Sudan amesema kuwa jeshi la nchi hiyo imezima majaribio kadhaa ya mapinduzi.

Akizungumza na gazeti la al Sharq al Ausat kuhusu madai ya kufanyika jaribio la mapinduzi baada ya kuondolewa madarakani serikali ya Omar al Bashir nchini Sudan, Abdul Fattah al Burhan amesema kuwa: Hadi sasa kumefanyika majaribio kadhaa ya mapinduzi nchini lakini yote yamezimzwa na kushindwa. 

Vilevile amezungumzia suala la kutoa amri ya kuachiwa huru mateka, watu waliotiwa nguvuni katika machafuko ya ndani na kutolewa msamaha kwa watu waliohukumiwa kwa sababu za kisaisa na kusema: Watu wote waliohukumiwa kwa sababu za kisiasa wataachiwa huru hivi karibuni. 

Abdul Fattah al Burhan

Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito la Sudan amekiri kwamba baraza hilo linasaidiwa na kupata himaya ya Saudi Arabia, Imarati na Misri. Amesema kuwa Baraza la Kijeshi la Mpito litatia saini makubaliano ya amani na vyama vya kisiasa vya upinzani baada ya kukamilka kazi ya kutayarisha hati ya muundo wa serikali ya mpito. 

Itakumbukwa kwamba, Alkhamisi iliyopita wawakilishi wa Baraza la Kijeshi la Mpito nchini Sudan walifikia makubaliano ya kugawana madaraka na kuunda serikali ya mpito nchini humo chini ya upatanishi wa Umoja wa Afrika na Ethiopia.