Machafuko yasababisha kufungwa shule nchini Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i55100-machafuko_yasababisha_kufungwa_shule_nchini_sudan
Muhyiddin al Jaali Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Malezi ya Sudan ameagiza kufungwa shule kote nchini humo baada ya kuuawa wanafunzi kadhaa katika maandamano ya Jumatatu wiki hii.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 31, 2019 03:45 UTC
  • Machafuko yasababisha kufungwa shule nchini Sudan

Muhyiddin al Jaali Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu na Malezi ya Sudan ameagiza kufungwa shule kote nchini humo baada ya kuuawa wanafunzi kadhaa katika maandamano ya Jumatatu wiki hii.

Wafanya maandamano watano wakiwemo wanafunzi wanne waliuawa juzi Jumatatu katika ghasia zilizoibuka katika mji wa al Obeid kaskazini mwa mkoa wa Kordofan huko Sudan. Wanafunzi waliandamana kulalamikia uhaba wa mafuta na mkate. Hali ya mgogoro ilianza kuikumba Sudan tangu Disemba 19 mwaka jana wakati wananchi walipoandamana pakubwa kulalamikia hali mbaya ya kiuchumi na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali khususan bei ya mkate na petroli. Maandamano hayo ya wananchi wa Sudan yaliingiliwa na askari usalama na hivyo kusababisha taathira kubwa za kisiasa, kiuchumi na kiusalama kutokana na ukandamizaji unaofanywa na askari hao. 

Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Mpito la Sudan lilichukua hatamu za uongozi baada ya jeshi kufanya mapinduzi na kumuondoa marakani Rais Omar al Bashir Aprili 11 mwaka huu; hata hivyo wananchi wangali wanaandamana wakishinikiza kuundwa serikali ya kiraia huko Sudan. 

Viongoi wa Baraza la Kijeshi la Sudan