Sudan yazikosoa Saudia na Imarati kwa kushindwa kutekeleza ahadi zao za kifedha
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i56507-sudan_yazikosoa_saudia_na_imarati_kwa_kushindwa_kutekeleza_ahadi_zao_za_kifedha
Waziri wa Fedha wa Sudan amezikosoa Saudia na Imarati kwa kushindwa kutekeleza ahadi zao za kifedha kuihusu nchi hiyo.  
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 09, 2019 03:56 UTC
  • Sudan yazikosoa Saudia na Imarati kwa kushindwa kutekeleza ahadi zao za kifedha

Waziri wa Fedha wa Sudan amezikosoa Saudia na Imarati kwa kushindwa kutekeleza ahadi zao za kifedha kuihusu nchi hiyo.  

Ibrahim al-Badawi, aliyasema hayo Jumanne ya jana na kuongeza kuwa Saudia na Imarati zimeweza tu kutoa nusu ya msaada zilioahidi kutoa wa Dola bilioni tatu kwa Sudan, msaada ambao ziliahidi mwezi Aprili mwaka huu. Hii ni katika hali ambayo awali Riyadh na Abu Dhabi ziliahidi kuipatia msaada wa kifedha serikali ya Sudan wenye lengo la kuiokoa nchi hiyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi unaoikabili.

Wakati makamanda wa kijeshi wa Sudan walipopewa ahadi hewa na watawala wa Saudia na Imarati

Waziri wa Fedha wa Sudan amesema kuwa katika ahadi zao Saudi Arabia na Imarati zimetoa kiasi cha Dola milioni 500 kama amana kwa benki kuu ya nchi hiyo huku kiasi kingine kikiwa ni katika kudhamini mahitaji ya nishati ya mafuta, ngano na mazao mengine ya kilimo. Inafaa kuashiria kuwa, tangu kipindi cha uongozi wa Omar al-Bashir, rais wa zamani wa Sudan, serikali ya Khartoum ilikubali kutuma mamia ya askari wake kwenda kujiunga na muungano vamizi wa Saudia na Imarati katika kuishambulia Yemen, mkabala wa kupewa fedha na nchi hizo vamizi.