Khalifa Haftar aainisha masharti kwa ajili ya kuanza mazungumzo huko Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i61420-khalifa_haftar_aainisha_masharti_kwa_ajili_ya_kuanza_mazungumzo_huko_libya
Kamanda wa kundi kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya ameainisha masharti ili kufanya mazungumzo na serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 04, 2020 22:20 UTC
  • Khalifa Haftar aainisha masharti kwa ajili ya kuanza mazungumzo huko Libya

Kamanda wa kundi kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya ameainisha masharti ili kufanya mazungumzo na serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo.

Khalifa Haftar kamanda wa kundi la wanamgambo kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya amnbaye yuko ziarani mjini Cairo amesema kuwa jeshi la Uturuki linaingilia moja kwa moja katika mapigano huko Libya na akasema kabla ya kufanya mazungumzo na serikali ya umoja wa kitaifa wanajeshi wa Uturuki wanapasa kuondoka Libya. 

Jenerali haftar ameongeza kuwa hakutakuwa na mazungumzo yoyote kabla ya kurudi nyuma wanamgambo wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya. 

Khalifa Haftar ametaka jeshi la kitaifa la Libya liondolewe  vikwazo vya silaha. Amesema Misri inapasa kuuungwa mkono kimataifa ili kukabiliana na ushawishi wa Uturuki huko Libya. Kabla ya hapo, Muhammad Qanunu Msemaji wa vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya alitangaza kuwa vikosi vya serikali hiyo vimefanikiwa kuudhibiti mji mkuu Tripoli. 

Kanali Muhammad Qanunu 

Itakumbukwa kuwa Misri, Imarati, Saudi Arabia na Ufaransa zinawaunga mkono wanamgambo wa Khalifa Haftar huku Uturuki, Qatar, Italia na Umoja wa Mataifa zikiiunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya yenye makao yake Tripoli.