Spika wa Bunge la Tunisia asisitiza ushirikiano zaidi na Uturuki
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i62580-spika_wa_bunge_la_tunisia_asisitiza_ushirikiano_zaidi_na_uturuki
Spika wa Bunge la Tunisia amefanya mazungumzo na mwenzake wa Uturuki ambapo ametoa wito wa kuimarishwa uhusiano wa nchi hizo mbili.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Aug 02, 2020 22:59 UTC
  • Spika wa Bunge la Tunisia asisitiza ushirikiano zaidi na Uturuki

Spika wa Bunge la Tunisia amefanya mazungumzo na mwenzake wa Uturuki ambapo ametoa wito wa kuimarishwa uhusiano wa nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa taarifa, Rached Ghannouchi, Spika wa Bunge la Tunisia katika mazungumzo ya simu na Spika wa Bunge la Uturuki Mustafa Sentop amesema: "Tunajitahidi kuimarisha uhusiano na Ankara." Kwa upande wake Mustafa Sentop amesema: "Tunafuatilia kwa karibu matukio ya kisiasa ya Tunisia na kwa kuzingatia hali ya Libya, msimamo wa kisiasa wa serikali ya Tunisia ni muhimu sana kwetu."

Sentop aidha ameelezea matumaini kuwa, hivi karibuni Ghanouchi atatembelea Uturuki akiwa na wabunge wa Tunisia.

Spika wa Bunge la Uturuki Mustafa Sentop

Serikali ya Uturuki inaunga mkono Serikali ya Muafaka wa Kitaifa ya Libya (GNU) ambayo hivi sasa inakabiliwa na hujuma za wanamgambo wa jenerali muasi Khalifa Haftar ambaye anapata himaya ya Misri, Imarati, Saudia na baadhi ya nchi za Ulaya.

Kufuatia msaada wa Uturuki, wanajeshi wa Serikali ya Muafaka wa Kitaifa ya Libya katika siku za hivi karibuni wamefanikiwa kutoa pigo kubwa kwa wanamgambo wa Haftar.