Watunisia wasisitiza kuhuishwa uhusiano na Syria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i63643-watunisia_wasisitiza_kuhuishwa_uhusiano_na_syria
Jumuiiya ya Kitaifa ya Kuunga mkono Muqawama na kupambana na utawala wa Kizayuni ya Tunisia imefanya maandamano na kusisitiza kuanzishwa tena uhusiano kati ya nchi hiyo na Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 25, 2020 23:24 UTC
  • Watunisia wasisitiza kuhuishwa uhusiano na Syria

Jumuiiya ya Kitaifa ya Kuunga mkono Muqawama na kupambana na utawala wa Kizayuni ya Tunisia imefanya maandamano na kusisitiza kuanzishwa tena uhusiano kati ya nchi hiyo na Syria.

Akizungumza na shirika rasmi la habari la Syria (SANA), Ahmed al Kahlawi  ameeleza kuwa, wananchi wa Tunisia wamefanya juhudi kubwa za kuanzishwa tena uhusiano kati ya nchi hiyo na Syria na wanaunga mkono ushindi ilioupata nchi hiyo katika mapambano dhidi ya ugaidi wa kimataifa na waungaji mkono wake. 

Al Kahlawi aidha amevitaja vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Syria viitwavyo " Caesar" kuwa ni uhalifu wa kinyama dhidi ya watu Syria na kusistiza kuwa, vikwazo hivyo vitashindwa tu kwa azma thabiti ya taifa hilo, uongozi na jeshi la nchi hiyo sawa kabisa kama yalivyogonga mwamba mashambulizi dhidi ya Syria. Mkuu wa Jumuiya ya Kitaifa ya Kuunga mkono Muqawama na kukabiliana na utawala wa Kizayuni ya Tunisia amesema kuwa siku chache zijazo jumuiya hiyo itaitisha maandamano ya kuonyesha mshikamano na Syria kwa kushirikiana na tawi la Umoja wa Kitaifa la Wanachuo wa nchi hiyo kwenye mji mkuu wa Tunisia, Tunis.  

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League)

Itakumbukwa kuwa, mwaka 2011 baada ya kuibuka mgogoro huko Syria, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) ilisimamisha uwanachama wa Syria ndani ya jumuiya hiyo kufuatia mashinikizo ya Saudi Arabia na kisha aghalabu ya nchi za Kiarabu zikakata uhusiano wao wa kidiplomasia na Damascus na kufunga balozi zao nchini Syria.