Vyama na shakhsia wa Tunisia walaani kuuliwa kigaidi Shahidi Fakhrizadeh
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i64939-vyama_na_shakhsia_wa_tunisia_walaani_kuuliwa_kigaidi_shahidi_fakhrizadeh
Vyama na shakhsia mbalimbali nchini Tunisia wametoa taarifa na kulaani mauaji ya kigaidi ya Shahidi Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi mkubwa wa nyuklia na masuala ya ulinzi wa Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 01, 2020 01:02 UTC
  • Vyama na shakhsia wa Tunisia walaani kuuliwa kigaidi Shahidi Fakhrizadeh

Vyama na shakhsia mbalimbali nchini Tunisia wametoa taarifa na kulaani mauaji ya kigaidi ya Shahidi Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi mkubwa wa nyuklia na masuala ya ulinzi wa Iran.

Chama cha Harakati ya Wananchi wa Tunisia jana Jumatatu kilitoa taarifa iliyosainiwa na Muhamad Zahir Katibu Mkuu wa chama hicho na kulaani mauaji ya kigaidi ya Fakhrizadeh mwanasayansi mkubwa wa nyuklia na masuala ya ulinzi wa Iran. Chama hicho kimeyataja mauaji hayo kuwa jinai kubwa iliyotekelezwa na magenge ya Kizayuni na kuongeza kuwa hiyo ni jinai mpya ambayo imefanywa na magaidi za Kizayuni dhidi ya wanasayansi wa Kiislamu na Kiarabu kwa lengo la kukwamisha maendeleo ya nchi za eneo ikiwemo kupatikana mlingano wa kistratejia dhidi ya utawala wa Kizayuni.  

Wananchi wa Iran wakilaani mauaji ya mwanasansi mkubwa wa nyuklia wa Iran

Chama cha Harakati ya Wananchi wa Tunisia kimeongeza kuwa, kinalaani vikali jinai hiyo kuu iliyotekelezwa na adui Mzayuni na kuutolea wito mhimili wa muqawama  kujibu jinai hiyo kwa uwezo wake wote.  

Kituo cha Amani na Mshikamano cha Tunisia pia kimetoa taarifa na huku kikilaani jinai hiyo kimetangaza kuwa ubeberu wa Marekani na mrengo wa Kizayuni na vibaraka wao wanaendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya wananchi walio huru ambao hawako tayari kupiga magoti na kusalimu amri mbele ya matakwa yao.   

Wakati huo huo Abdul Latif al Makki mwanasiasa na tabibu wa nchini Tunisia ambaye ndiye mkuu wa Harakati ya An Nahdhah ya nchini humo pia amelaani mauaji hayo ya kigaidi ya shahidi Mohsen Fakhrizadeh mwanasayansi wa nyuklia na masuala ya ulinzi wa Iran  na kutoa mkono wa pole kwa wananchi na familia ya mwendazake huyo. Ameongeza kuwa, hii si mara ya kwanza kuona mwanasayansi wa Kiirani anauliwa kigaidi  bali kabla ya mauaji haya pia aghalabu ya wanasayansi wa Iran wameuliwa kigaidi na uistikbari wa Magharibi.  

Mamluki wa kigaidi waliokuwa na silaha Ijumaa iliyopita walishambulia gari lililokuwa limembeba Mohsen Fakhrizadeh Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu wa Wizara ya Ulinzi ya Iran na  kumuua shahidi. Hadi sasa nchi kadhaa duniani zikiwemo Russia, Venezuela, Afrika Kusini, Imarati, Uswisi, Jordan na Uturuki pia zimelaani mauaji ya kigaidi ya Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi mkubwa wa nyuklia na masuala ya ulinzi wa Iran.