Aug 11, 2021 03:46 UTC
  • Moto wauawa watu 7 katika misitu ya Algeria

Kwa akali watu saba wamepoteza maisha baada ya moto mkubwa kuteketeza misitu katika mkoa wa Tizi Ouzou nchini Algeria.

Mamlaka ya Ulinzi wa Raia nchini humo imesema katika taarifa ya jana Jumanne kuwa, mbali na watu saba kupoteza maisha kutokana moto huo wa misituni, lakini wengine wawili wamejeruhiwa vibaya.

Taarifa ya mamlaka hiyo imeogeza kuwa, akthari ya nyumba zilizokuwa zinapakana na misitu inayoteketea moto katika mkoa huo ulioko yapata kilomita 150 mashariki mwa mji mkuu Algiers, zimebakia majivu kutokana na moto huo.

Gazeti la al-Bilad la nchi hiyo limeripoti kuwa, shule za mkoa wa Tizi Ouzou zinawapokea wananchi waliolazimika kuwa wakimbizi wa ndani kutokana na mkasa huo wa moto wa misituni.

Nchi nyingi duniani hivi sasa zinashuhudia visa vya moto kuwaka misituni

Habari zaidi zaidi zinasema kuwa, visa 19 vya misitu kuteketea kwa moto vimeripotiwa katika mikoa 14 ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika katika siku za hivi karibuni.

Kwa wiki kadhaa sasa, mioto mikubwa inaendelea kuteketeza misitu huko Marekani haswa katika jimbo la California na vile vile katika nchi za Ulaya hususan Ugiriki. Uturuki imepata ahueni baada ya mvua kunyesha na kuzima moto uliokuwa ukiteketeza misitu katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. 

Tags