Haftar aafiki kutimuliwa mamluki 300 wa kigeni nchini Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i76814-haftar_aafiki_kutimuliwa_mamluki_300_wa_kigeni_nchini_libya
Wawakilishi wa Jenerali mstaafu Khalifa Haftar katika kamati ya kijeshi inayojulikana kwa jina la kundi la 5+5 huko Libya wamesema kuwa wameafiki kuondolewa wapiganaji mamluki 300 wa kigeni katika maeneo yanayodhibitiwa la kundi la linalojiiita Jeshi la Taifa la Libya.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 12, 2021 07:52 UTC
  • Haftar aafiki kutimuliwa mamluki 300 wa kigeni nchini Libya

Wawakilishi wa Jenerali mstaafu Khalifa Haftar katika kamati ya kijeshi inayojulikana kwa jina la kundi la 5+5 huko Libya wamesema kuwa wameafiki kuondolewa wapiganaji mamluki 300 wa kigeni katika maeneo yanayodhibitiwa la kundi la linalojiiita Jeshi la Taifa la Libya.

Afisa mmoja wa kundi la Jenerali Haftar amesema kuwa wapiganaji hao wa kigeni watakuwa kundi la kwanza la mamluki kuondoka Libya kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa mwezi uliopita na pande mbili hasimu chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

Afis huyo amesema hatua hiyo itaimarisha zaidi makubaliano hayo na kwamba kuondolewa wapiganaji mamluki nchini Libya kutafanyika kwa ushirikiano wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo ili kuepusha machafuko katika nchi zao.

Afrika huyo wa kundi la Jenerali Haftar hakutaja kajina ya nchi wanakotokea mamluki hao lakini amesisitiza kuwa operesheni hiyo itafanyika kwa ushirikiano na nchi jirani. Tangazo hiyo la kundi la Jenerali Khalifa Haftar limetolewa siku moja kabla ya mkutano wa kimataifa wa amani ya Libya unaofanyika leo katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Mkutano huo umeitishwa ili kuonesha uungaji mkono wa jamii ya kimataifa kwa hatua zilizochukuliwa za kuitisha uchaguzi mkuu nchini Libya na kuwaonya wale wote wenye nia ya kukwamisha zoezi hilo.     

Hatimaye baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo na vuta nikuvute baina ya makundi na mirengo tofauti ya kisiasa nchini Libya, uandikishaji majina ya wagombea wa kiti cha Rais na Bunge ulianza Jumatatu ya tarehe 8 mwezi huu wa Novemba.

Zoezi la uandikishaji majina ya wagombea wa viti vya Ubunge litaendelea hadi tarehe 7 ya mwezi ujao wa Disemba ilihali zoezi la kuandikisha wagombea Urais pazia lake litafungwa tarehe 22 ya mwezi huu wa Novemba.

Abdul-Hamid Dbeibah Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Jenerali Khalifa Haftar, mbabe mkuu wa vita vya ndani nchini Libya na Saif al-Islam Gaddafi, mwana wa kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi ni miongoni mwa wanaotazamiwa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha rais wa Libya.