Mripuko wa bomu watikisa viungani mwa mji mkuu wa Misri, Cairo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i7849-mripuko_wa_bomu_watikisa_viungani_mwa_mji_mkuu_wa_misri_cairo
Idadi kubwa ya watu wanahofiwa kupoteza maisha katika mripuko wa bomu ulioutikisa mji wa Giza, ambao uko karibu na mji mkuu wa Misri, Cairo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 26, 2016 03:36 UTC
  • Mripuko wa bomu watikisa viungani mwa mji mkuu wa Misri, Cairo

Idadi kubwa ya watu wanahofiwa kupoteza maisha katika mripuko wa bomu ulioutikisa mji wa Giza, ambao uko karibu na mji mkuu wa Misri, Cairo.

Habarin zinasema kuwa, mripuko huo umetokea katika mtaa wa Tahrir, eneo la al-Doqi , katika mji wa Giza ulioko umbali wa kilomita 20, kusini magharibi mwa mji mkuu Cairo.

Mashuhuda wamesema wamesikia sauti kubwa na ya kishindo ya mripuko katika eneo hilo na yumkini umesababisha maafa na uharibifu mkubwa. hata hivyo hawajataja idadi ya mejeruhi wala walioaga katika mripuko huo unaoaminika kuwa wa bomu.

Haya yanajiri siku moja baada ya Jeshi la Misri kutangaza kuwa, limefanikiwa kuua magaidi wasiopungua 85 katika kipindi cha siku nne zilizopita kwenye maeneo ya Sheikh Zuweid na Rafah, katika rasi ya Sinai ya kaskazini mwa nchi hiyo. Tangu miezi kadhaa iliyopita, jeshi la Misri lilianzisha operesheni kubwa katika maeneo ya Rafah, Sheikh Zuweid na al Aris huko Sinai Kaskazini kwa lengo la kuyamaliza magenge hayo ya kigaidi.