Wanajeshi saba wa serikali ya Libya wauawa Sirte
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i7972-wanajeshi_saba_wa_serikali_ya_libya_wauawa_sirte
Wanajeshi saba wa serikali ya Libya wameuliwa katika mapigano na kundi la kitakfiri na Kizayuni la Daesh karibu na mji wa Sirte.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 28, 2016 03:24 UTC
  • Wanajeshi saba wa serikali ya Libya wauawa Sirte

Wanajeshi saba wa serikali ya Libya wameuliwa katika mapigano na kundi la kitakfiri na Kizayuni la Daesh karibu na mji wa Sirte.

Wanajeshi saba wenye mfungamano na Baraza la Uongozi la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya jana waliuawa na wengine 25 kujeruhiwa katika mapigano na kundi la kitakfiri na Kizayuni la Daesh karibu na mji wa Sirte nchini humo.

Chumba cha oparesheni za kundi hilo la "Al Bunyan -Marsus" kimetangaza kuwa vikosi vya anga vyenye mfungamano na akademia ya kijeshi ya mji wa Misrata vilishiriki kwenye oparesheni hiyo katika mashambulizi dhidi ya ngome za Daesh.

Ripoti zinasema kuwa kundi la kitakfiri la Daesh limepoteza zana zake nyingi za kijeshi na kupata kipigo kikubwa kutoka vikosi vya serikali ya Libya katika mapigano kati ya pande hizo kusini mashariki mwa mji wa Abu Qarin na vile vile huko mashariki mwa mji wa Misrata kuelekea katika mji wa Sirte.

Chumba cha oparesheni kwa jina la Al Bun'yan Marsus kiliasisiwa tarehe 5 mwezi huu kwa agizo la Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya Fayez al Siraj kwa minajili ya kuratibu ushirikiano kati ya brigedi za mapambano zenye mfungamano na serikali ya nchi hiyo.