Polisi watatu watiwa mbaroni nchini Misri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8080-polisi_watatu_watiwa_mbaroni_nchini_misri
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Misri ametoa amri ya kutiwa mbaroni maafisa watatu wa jeshi la polisi la nchi hiyio kwa tuhuma za kumtesa na kumpiga vibaya raia mmoja wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 30, 2016 00:05 UTC
  • Polisi watatu watiwa mbaroni nchini Misri

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Misri ametoa amri ya kutiwa mbaroni maafisa watatu wa jeshi la polisi la nchi hiyio kwa tuhuma za kumtesa na kumpiga vibaya raia mmoja wa nchi hiyo.

Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, maafisa hao watatu wa polisi wamempiga na kumjeruhi vibaya raia mmoja wa nchi hiyo na kusababisha kifo chake.

Hii ni kesi ya karibuni kabisa ya uhalifu unaofanywa na maafisa wa polisi wa Misri dhidi ya raia wa nchi hiyo.

Shirika la Haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kuwa, polisi wa Misri wanawatesa vibaya wafungwa, kama ambavyo limewatuhumu polisi wa nchi hiyo kwa kuwafunga na kuwapa mateso makali watu 20 wakiwemo watoto wanane.

Ripoti ya Human Rights Watch imewanukuu baadhi ya wafungwa wakisema kuwa, jeshi la polisi la Misri linawatesa wa kuwaning'iniza kichwa chini miguu juu na kuwapiga, kuwatukana pamoja na kuwachoma kwa shoti za umeme.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kutiwa mbaroni maafisa hao watatu wa polisi kunazidi kufichua vitendo viovu vinavyofanywa na jeshi la polisi la Misri dhidi ya raia.