Rais wa zamani wa Tunisia ataka kususiwa kura ya maoni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i85210-rais_wa_zamani_wa_tunisia_ataka_kususiwa_kura_ya_maoni
Moncef al Marzouq Rais wa zamani wa Tunisia amewatolea wito wananchi kususia kura ya maoni kuhusu katiba ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 26, 2022 23:15 UTC
  • Rais wa zamani wa Tunisia ataka kususiwa kura ya maoni

Moncef al Marzouq Rais wa zamani wa Tunisia amewatolea wito wananchi kususia kura ya maoni kuhusu katiba ya nchi hiyo.

Al Marzouq amesema anawatolea wito wananchi wa Tunisia kususia kura hiyo tarajiwa ya maoni kuhusu katiba mpya ya Tunisia. Moncef al Marzouq alikuwa Rais wa Tunisia kuanzia mwaka 2011 hadi 2014. Kabla ya al Marzouq kutoa wito huo, Rashed al Ghanouchi Spika wa Bunge la Tunisia aliyefukuzwa ambaye ni mkuu wa Chama cha Kiislamu cha nchini humo cha An Nahadhah pia alitoa wito wa kususiwa kura hiyo tarajiwa ya maoni. 

Rais Kais Saeid wa Tunisia ametangaza kuwa, kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya nchi hiyo itafanyika Julai 25 mwaka huu. 

Rais Kais Saeid wa Tunisia 

Rais wa Tunisia Juni 25 mwaka jana alichukua madaraka ya Tunisia kwa kutekeleza hatua kadhaa za aina yake ambapo alisimamisha Bunge na kumfuta kazi spika wake, pamoja na waziri mkuu wa serikali, na kuchukua udhibiti wa mambo yote ya nchi. Hatua ya Rais Saed ya kuifuta kazi serikali ilisababisha mkwamo mkubwa wa kisiasa nchini humo ulioibua malalamiko na upinzani wa vyama na mirengo mbalimbali ya kisiasa khususan chama cha An Nahadhah.  

Wapinzani wa Rais Kais Saeid wanamtuhumu kwa kufanya mapinduzi dhidi ya mafanikio ya kidemorasia yaliyopatikana katika vuguvugu la mapambano ya mwaka 2011 yaliyomuondoa madarakani Rais Zainul Abidin bin Ali,  hata hivyo Kais Saeid anasema, hatua alizochukua ni halali na kwamba kulikuwa na udharura wa kufanya hivyo ili kuinusuru Tunisia katika dimbwi la mgogoro wa kisiasa wa muda mrefu.