Nov 26, 2022 02:33 UTC
  • Ghana kuipiga kando dola ya Marekani katika ununuzi wa mafuta

Serikali ya Ghana inaanda sera mpya ya kununua bidhaa za mafuta kwa kutumia dhahabu badala ya sarafu ya dola ya Marekani.

Makamu wa Rais wa Ghana, Mahamudu Bawumia amesema katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa Facebook kuwa: Iwapo mpango huu utatekelezwa barabara kama ilivyopangwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2023, tutabadilisha mlingano wa mbinu za malipo na tupungeze kushuka kwa thamani ya sarafu yetu.

Mpango huo unakusudia kukabiliana na suala la kupungua kwa akiba ya sarafu za kigeni nchini humo, hatua ambayo mbali na kusababisha kuendelea kupoteza thamani sarafu ya Cedi ya Ghana, lakini pia imepelekea kuongezeka kwa gharama za maisha nchini humo.

Makamu wa Rais wa Ghana amefafanua kuwa, kutumia dhahabu kulipia bidhaa za mafuta zinazoagizwa na nchi hiyo kutazuia bei ya safaru za kigeni kuathiri bei za mafuta na bidhaa nyingine nchini humo.

Ameeleza kuwa, kwa kutumia dhahabu, wauzaji wa bidhaa za mafuta nchini humo hawatalazimika tena kuagiza bidhaa hizo kwa kutegemea kupanda na kushuka kwa sarafu ya dola.

Ghana inazalisha mafuta ghafi, lakini inategemea bidhaa za mafuta yaliyosafishwa kutoka nje, tangu kiwanda chake cha kusafisha mafuta kifungwe mwaka 2017, kutokana na mripuko.

 

 

Tags