Wazayuni waliojipenyeza kilaghai kikao cha AU watimuliwa kidhalili na askari wa Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i94210-wazayuni_waliojipenyeza_kilaghai_kikao_cha_au_watimuliwa_kidhalili_na_askari_wa_afrika
Ujumbe wa utawala waw Kizayuni ulioingia kilaghai katika kikao cha Umoja wa Afrika umetimuliwa kidhalili na kifedheha na askari wa Umoja wa Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 18, 2023 22:57 UTC
  • Wazayuni waliojipenyeza kilaghai kikao cha AU watimuliwa kidhalili na askari wa Afrika

Ujumbe wa utawala waw Kizayuni ulioingia kilaghai katika kikao cha Umoja wa Afrika umetimuliwa kidhalili na kifedheha na askari wa Umoja wa Afrika.

Kikao cha 36 cha Umoja wa Afrika AU kilianza tarehe 15 mwezi huu wa Februari na kitaendelea hadi Februari 19 katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Kikao hicho cha ngazi za juu kinawajumuisha pamoja wakuu na maafisa waandamizi wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, mawaziri wa nchi wanachama na wakuu wa asasi na ofisi mbalimbali za umoja huo. 

Shirika la habari la FARS liliripoti jana (Jumamosi) kuwa, askari wa kulinda usalama wa Umoja wa Afrika wameutimua ujumbe wa utawala wa Kizayuni wa Israel uliongia kilaghai kwenye kikao hicho kwa kutumia majina bandia na vitambulisho vya watu wengine. 

Bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Wazayuni wanadai kuwa walialikwa kwenye kikao cha ufunguzi lakini wameshindwa kutoa uthibitisho wowote hivyo wamefukuzwa kifedheha kwenye kikao hicho. 

Kutimuliwa kidhalili ujumbe huo wa Wazayuni katika kikao cha AU kunazidi kuthibitisha jinsi jinai za Israel zinavyowakasirisha watu wenye fikra huru ulimwenguni.

Mwaka 2021, mkuu wa Kamisheni ya Afrika ya AU alijitangazia mwenyewe tu kuwa utawala wa Kizauni ni mwanachama mwangaliaji wa vikao vya umoja huo. Hatua hiyo ililalamikiwa vikali na nchi za Afrika zikiwemo Algeria na Afrika Kusini. Ndio maana mwezi Februari 2022, Wazayuni walifukuzwa rasmi kwenye vikao vya Umoja wa Afrika.