Umoja wa Ulaya waahidi kushirikiana na Afrika Magharibi dhidi ya ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9910-umoja_wa_ulaya_waahidi_kushirikiana_na_afrika_magharibi_dhidi_ya_ugaidi
Umoja wa Ulaya umesema kuwa utashirikiana na nchi za eneo la Magharibi mwa Afrika katika vita dhidi ya ugaidi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 25, 2016 06:25 UTC
  • Umoja wa Ulaya waahidi kushirikiana na Afrika Magharibi dhidi ya ugaidi

Umoja wa Ulaya umesema kuwa utashirikiana na nchi za eneo la Magharibi mwa Afrika katika vita dhidi ya ugaidi.

Kamati ya Stratejia ya Umoja wa Ulaya (COS) jana ilitangaza kuwa imedhamiria kwa dhati kustafidi na nyenzo zinazofaa katika kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi ili kudumisha amani na uthabiti katika eneo.

Kamati hiyo ya Umoja wa Ulaya iliyatamka hayo jana baada ya kumalizika kkikao chake cha tatu kuhusu masuala ya Magharibi mwa Afrika huko Lome mji mkuu wa Togo.

Kamati hiyo ya Umoja wa Ulaya imesema inasikitishwa na kushadidi mashambulizi ya kigaidi katika eneo la magharibi mwa Afrika ikiwemo huko Burkina Faso, Ivory Coast, Niger na Nigeria na kutangaza mshikamano wake na nchi zilizoathirika na mashambulizi hayo.

Kamati ya Stratejia ya Umoja wa Ulaya pia imebainisha kuwa ni jambo lisilowezekana kuwepo ustawi katika eneo la Magharibi mwa Afrika bila ya kurejeshwa amani na uthabiti katika eneo.

Kamati hiyo imesisitiza kuzisimamia idara za kiufundi za umoja huo, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (CEDEAO), na Jumuiya ya Uchumi na Fedha ya Magharibi mwa Afrika (UEMOA) kuhusu ubadilishanaji wa taarifa kati ya idara za usalama za eneo.