-
Sheikh Zakzaky aipongeza Iran kwa kuibuka mshindi dhidi ya Israel
Jul 06, 2025 11:12Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amepongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuichakaza na kuibuka mshindi dhidi ya Israel katika vita vya siku 12.
-
Waislamu wa Kenya watishia kujitenga na Mfumo wa sheria kupinga hukumu ya urithi
Jul 06, 2025 11:03Viongozi wa Kiislamu nchini Kenya wameonya kuwa huenda jamii yao ikajitenga na mfumo wa kisheria wa nchi hiyo iwapo serikali haitachukua hatua ya kufuta au kurekebisha hukumu ya Mahakama ya Juu kuhusu haki ya watoto waliozaliwa nje ya ndo kurithi mali.
-
MSF: Huduma za afya nchini Sudan zinasitishwa, mashambulizi kwenye vituo vya afya yanaongezeka
Jul 05, 2025 23:46Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanaendelea kupaza sauti juu ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya nchini Sudan, yakionya kwamba asilimia 70 kati ya vituo hivyo vimefungwa au vinafanya kazi kwa shida.
-
Equatorial Guinea yaishtaki Ufaransa kwa mahakama ya UN kwa uporaji
Jul 05, 2025 11:53Equatorial Guinea imewasilisha kesi dhidi ya Ufaransa katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ikitaka kusitishwa uuzaji wa jumba la kifahari mjini Paris, ambalo nchi hiyo ya Afrika Magharibi inataka kulitwaa tena, mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa ilisema hayo jana Ijumaa.
-
Rais wa Rwanda asema hana uhakika wa kufanikiwa makubaliano ya amani ya DRC
Jul 05, 2025 03:49Rais Paul Kagame wa Rwanda amekaribisha kwa tahadhari makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na kundi la waasi la M23 kwa upatanishi wa Marekani akisema, kufanikiwa kwa mapatano hayo kunategemea nia njema itakayoonyeshwa na pande husika.
-
Rais Ruto akiri kujenga kanisa ndani ya Ikulu ya Rais, asema: Sitaomba msamaha
Jul 04, 2025 11:53Rais William Ruto wa Kenya amekiri kuwa anajenga Kanisa katika Ikulu ya Rais akidai kuwa anatumia pesa zake kujenga kanisa hilo.
-
Rais wa Afrika Kusini: Mazungumzo ya kitaifa yataendelea bila mshirika wa muungano
Jul 04, 2025 11:49Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema kuwa mazungumzo ya kitaifa yenye lengo la kuimarisha umoja na kuiunganisha nchi baada ya uchaguzi wa mwaka jana yataendelea bila mshirika mkuu katika serikali ya mseto ya nchi hiyo.
-
Waasi wa M23: Tuko tayari kushiriki mazungumzo ya amani ya Doha
Jul 04, 2025 03:42Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na waasi wa M23 wamesema kwamba watatuma wajumbe nchini Qatar kwa mazungumzo ya amani, huku Washington ikishinikiza kukomeshwa kwa mapigano ambayo yanaweza kusaidia kufungua mabilioni ya uwekezaji katika madini.
-
Madaktari Wasio na Mipaka waonya kuhusu uhalifu dhidi ya raia al-Fasher Sudan
Jul 04, 2025 03:31Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) lina wasiwasi kuhusu uwezekano wa kutokea mashambulizi makubwa katika mji wa al-Fasher na umwagaji damu unaoweza kusababisha, huku mamia kwa maelfu ya raia wakiwa wamekwama katika mji huo.
-
Serikali ya Tanzania yakanusha madai ya kupanga kumpa sumu Tundu Lissu
Jul 04, 2025 00:15Serikali ya Tanzania imekanusha vikali tuhuma zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kudai kuwa zinaihusisha yenyewe na kiongozi wa upinzani, Tundu Antipas Lissu, katika mpango wa kumuwekea sumu mshtakiwa huyo.