-
Misri yafurahia kurejeshwa turathi nyingi zilizoibwa na Marekani
May 13, 2025 23:15Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetangaza habari ya kurejeshwa nchini humo kutoka Marekani turathi 25 za kihistoria na za kisanii, zilizotwaliwa enzi za ustaarabu wa kale wa Misri.
-
Kumalizika operesheni ya kijeshi Tripoli; Libya yaingia tena kwenye mgogoro
May 13, 2025 23:11Wizara ya Ulinzi ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya imetangaza kumalizika kwa mafanikio operesheni ya kijeshi huko Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo.
-
Somalia yasajili wapiga kura baada ya miaka 56 ya kutokuwa na upigaji kura
May 13, 2025 08:55Zaidi ya miaka 56 tangu raia wa Somalia katika upigaji kura wa moja kwa moja, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mipaka ya Somalia imeanzisha mchakato mkubwa wa kusajili wapiga kura.
-
Joto lasababisha madhara makubwa barani Afrika
May 13, 2025 08:54Ripoti mpya kuhusu “Hali ya Hewa Afrika 2024” iliyotolewa wiki hii na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO imeonya kwamba muongo wa joto zaidi kuwahi kushuhudiwa Afrika umeleta madhara makubwa kwa bara hilo.
-
Wanajeshi kadhaa Nigeria wauawa katika hujuma ya magaidi wa Boko Haram
May 13, 2025 08:52Kundi la kigaidi la Boko Haram limevamia kambi ya kijeshi katika eneo la Serikali ya Mitaa ya Marte, Jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria, na kuwaua wanajeshi kadhaa.
-
Milio ya risasi yasikika Tripoli baada ya mauaji ya kiongozi wa wanamgambo
May 13, 2025 03:33Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kukomeshwa haraka machafuko katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, huku watu wenye silaha wakifyatuliana risasi katika wilaya za kusini mwa mji huo baada ya mauaji ya kiongozi aliyekuwa na nguvu wa kundi moja la wanamgambo.
-
Rais Traoré wa Burkina Faso aikosoa vikali kamandi ya kijeshi ya Marekani barani Afrika
May 13, 2025 01:01Rais Ibrahim Traoré wa Burkina Faso amemkosoa vikali mkuu wa Kamandi ya Kijeshi ya Marekani barani Afrika kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi yake huku akisema kuwa Muungano wa Nchi za Sahel ulioundwa hivi karibuni ni “Mfano wa Mshikamano” barani Afrika.
-
Mshambulizi ya waasi wa RSF yaua raia 7 katika mji wa El-Fasher, Sudan
May 13, 2025 00:49Jeshi la Sudan lilisema Jumatatu kwamba wapiganaji wa kundi la waasi wa RSF wameua raia saba kwa shambulizi la makombora mjini El-Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini magharibi mwa Sudan.
-
Kwa nini vikosi vya usalama vya Ufaransa vimefukuzwa Algeria?
May 12, 2025 23:32Sambamba na kuongezeka mvutano kati ya Algeria na Ufaransa, serikali ya Algiers imechukua uamuzi wa kuwafukuza maafisa wawili wa kiintelijensia wa Ufaransa waliokuwa na pasipoti za kidiplomasia.
-
Waislamu Nigeria wawakumbuka Mashahidi wa Siku ya Quds
May 12, 2025 07:44Taasisi ya 'Wakfu wa Shuhada' ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imewakumbuka na kuwaenzi mashahidi 27 waliouawa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo wakati wa maandamano ya amani ya Siku ya Quds ya 2025 huko Abuja, na kusisitiza kujitolea kwao kwa kadhia ya Palestina.