-
Diop: Ukraine inachochea ukosefu wa utulivu barani Afrika
Apr 08, 2025 03:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Abdoulaye Diop amesema Ukraine inavuruga utulivu barani Afrika kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel barani humo.
-
Idadi ya waliofariki dunia kwa mafuriko DRC yaongezeka, vita vinaendelea
Apr 07, 2025 22:58Mbali na majanga ya ukosefu wa amani na vita baina ya makundi hasimu, majanga ya kimaumbile yanaikumba pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Watu wasiopungua 33 wamethibitishwa kufarikidunia kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakati juzi Jumapili idadi hiyo ilikuwa ni watu 22.
-
UN yaimarisha doria katika kambi za wakimbizi huku kukiwa na ongezeko la ghasia Sudan Kusini
Apr 07, 2025 22:58Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini sasa unashika doria usiku na mchana katika eneo la wakimbizi ambalo liko karibu na kituo chake cha kulinda amani kutokana na kuongezeka hali ya wasiwasi nchini kote.
-
Ubalozi wa Marekani wazingirwa na waaandamanaji nchini Mauritania
Apr 07, 2025 22:58Wananchi wenye hasira wa Mauritania wamefanya maandamano makubwa na kuuzingira ubalozi wa Marekani mjini Nouakchott wakilaani jinai za Israel katika Ukanda wa Ghaza na kushiriki kikamilifu Washington katika jinai hizo.
-
Balozi wa Israel nchini Ethiopia afukuzwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika
Apr 07, 2025 09:20balozi wa Israel nchini Ethiopia, Abraham Negussie, amefukuzwa katika Ukumbi wa Mandela katika makao makuu ya Umoja wa Afrika leo Jumatatu.
-
Rwanda yaanza kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi
Apr 07, 2025 09:19Rwanda leo, tarehe 7 Aprili, imeanza shughuli za kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi yaliyofanywa na wanamgambo wa kihutu wenye misimamo mikali.
-
Wananchi wa Morocco waandamana kulaani jinai za Israel Gaza
Apr 07, 2025 08:06Maelfu ya wananchi wa Morocco wamefanya maandamano makubwa katikati mwa mji mkuu wa Rabat kulaani mashambulio mapya ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Ripoti: Nigeria yapanga mashambulizi dhidi ya Wafuasi wa Sheikh Zakzaky jijini Abuja
Apr 07, 2025 03:55Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na tovuti ya Sahara Reporters, maafisa wa usalama wa Nigeria wanapanga mashambulizi dhidi ya makazi na mali za wafuasi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria (IMN).
-
Mafuriko yaua watu 22 katika mji mkuu wa DR Congo, Kinshasa, baada ya mvua kubwa
Apr 07, 2025 03:54Takriban watu 22 wamethibitishwa kufariki dunia katika jiji la Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), baada ya Mto Ndjili kufurika na kusababisha mafuriko makubwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa wiki.
-
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii: Bunge limekuwa paradiso ya walafi
Apr 06, 2025 10:07Baadhi ya raia wa Kenya wanaotumia mitandao ya kijamii wameeleza kukasirishwa na hatua ya wabunge na maseneta ya kujiongezea posho za usafiri kupitia marekebisho ya marupurupu kwa kima cha jumula cha Sh bilioni 4.4.