-
RSF yaua na kujeruhi makumi ya raia wa Sudan Kordofan Kusini
Apr 02, 2025 23:02Kwa akali raia 12 wa Sudan wameuawa katika mashambulizi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika Jimbo la Kordofan Kusini.
-
Serikali ya DRC na waasi wa M23 kufanya mazungumzo ya kwanza Aprili 9 nchini Qatar
Apr 02, 2025 07:08Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imepanga kufanya mazungumzo ya kwanza kabisa na kundi la waasi wa M23, April 9 mwaka huu katika mji mkuu wa Qatar, Doha kwa lengo la kufikia mwafaka wa kurejesha amani katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Burkina Faso na Niger kukutana mjini Moscow wiki hii
Apr 02, 2025 03:33Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Burkina Faso na Niger wiki hii wataelekea ziarani mjini Moscow, Russia. Nchi hizo za eneo la Sahel barani Afrika zinaizuru Moscow katika jitihada za kuimarisha uhusiano wao na Russia.
-
Viongozi wa upinzani Kenya wadai, Rais Ruto na washirika wake wanataka kuiteka IEBC
Apr 02, 2025 03:10Viongozi wa upinzani nchini Kenya wamepinga mchakato unaoendelea wa kuunda upya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), wakimshutumu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM, Raila Odinga kwa kuvuruga mchakato huo.
-
Vipaumbele vya Afrika wakati wa uenyekiti wa Afrika Kusini ndani ya G20
Apr 02, 2025 00:05Wataalamu na watunga sera waliohudhuria mkutano kuhusu vipaumbele vya Afŕika wakati wa Urais wa Afrika Kusini wa Kundi G20 wamesisitizia haja ya kuyapa kipaumbele mageuzi muhimu ambayo yatasaidia ustawi na maendeleo ya Afŕika na kutumiwa vizuri utajiri mkubwa wa rasilimali wa bara hilo.
-
Jeshi la Sudan laendelea kupata mafanikio El Fasher, mapigano yanaendelea El Obeid
Apr 01, 2025 23:33Vyanzo vya kijeshi vya Sudan vimetangaza kwamba jeshi la nchi hiyo linapiga hatua mpya kusini mwa El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, na kwamba wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) wameshambulia sehemu ya magharibi ya mji huo kwa mizinga.
-
Mufti wa Uganda ataka kupigwa marufuku TikTok nchini humo
Apr 01, 2025 07:09Mufti wa Uganda, Sheikh Shaaban Ramadhan Mubajje, ametoa mwito kwa serikali kuu kupiga marufuku programu ya mtandao wa kijamii wa TikTok nchini humo, ambayo anasisitiza kuwa inatumiwa na watu wasio na kazi kuwakashifu na kuwapaka matope watu wengine.
-
Lubanga, mbabe wa kivita aunda kundi jipya la waasi DRC
Apr 01, 2025 07:07Aliyekuwa kinara wa genge moja la waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Thomas Lubanga na ambaye alikuwa mtu wa kwanza kukamatwa na kufungwa jela na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), amezindua kundi jipya la waasi nchini humo.
-
Lassa yaua watu 118 Nigeria ndani ya miezi mitatu
Apr 01, 2025 07:05Homa ya Lassa imeua watu 118 nchini Nigeria katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu. Hayo yamesemwa na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha nchi hiyo ya Afrika Magharibi (NCDC).
-
Kamanda wa RSF akiri wamefukuzwa Khartoum Sudan, aapa kujipanga upya
Mar 31, 2025 23:17Kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) Mohamed Hamdan Dagalo amekiri kwamba kundi lake limetimuliwa mjini Khartoum, sehemu ya mji mkuu wa Sudan na kuitaja hatua aliyoiita ni ya kujiondoa kwa hiari, kuwa ni mbinu ya kujipanga upya na kurejea Omdurman, mji mwingine muhimu sana.