-
Jeshi la Sudan ladhibiti Ikulu ya Rais mjini Khartoum
Mar 21, 2025 09:05Vikosi vya Jeshi la Sudan vimedhibiti Ikulu ya Rais wa nchi hiyo mjini Khartoum leo Ijumaa na hivi sasa linawaandamana wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) ndani ya Suuq al Arabi katikati mwa Khartoum.
-
Rais wa Tunisia amfuta kazi Waziri Mkuu, Kamel Maddouri
Mar 21, 2025 08:19Rais wa Tunisia, Kais Saied amemfukuza kazi Waziri Mkuu, Kamel Maddouri na kumteua Waziri wa Vifaa na Makazi, Sara Zaafarani kushika nafasi yake.
-
Jeshi la Somalia laua magaidi 82 wa al-Shabaab
Mar 21, 2025 04:45Jeshi la Anga la Somalia kwa ushirikiano na Shirika la Taifa la Usalama (NISA) limeangamiza magaidi 82 wa kundi la al-Shabaab katika mashambulizi ya anga katika eneo la Lower Shabelle.
-
Nigeria yaanza uchunguzi wa NGOs zilizofadhiliwa na USAID zinazodaiwa kuunga mkono ugaidi
Mar 21, 2025 04:39Wakaguzi wa Nigeria wameanzisha uchunguzi kuhusu shughuli za zaidi ya mashirika kumi yasiyo ya kiserikali, NGO, huku kukiwa na madai kwamba fedha za shirika la misaada la serikali ya Marekani, USAID, zilitumika kufadhili ugaidi nchini Nigeria.
-
Nchi Zaidi za Afrika zajiondoa katika Jumuiya ya Nchi Zinazozungumza Kifaransa
Mar 21, 2025 04:35Burkina Faso na Mali zimejitoa kutoka Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi Zinazozungumza Kifaransa (OIF), zikifuata mfano wa jirani wao wa Magharibi mwa Afrika, Niger, ambayo ilitangaza mapema kuondoka kwenye kundi hilo lenye makao yake mjini Paris.
-
Waasi wa M23 wauteka mji wa Walikale mashariki mwa Kongo DR
Mar 20, 2025 23:53Kundi la waasi la M23, linaloendesha mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limeuteka mji wa Walikale unaopatikana katika eneo lenye utajiri mkubwa wa madini huko Kivu Kaskazini.
-
Mapigano makali katika mji mkuu wa Sudan na karibu na ikulu ya Rais
Mar 20, 2025 06:47Duru za habari zimetangaza kuwa mapigano makali yamejiri kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum na karibu na ikulu ya Rais.
-
Mashambulizi ya Marekani Yemen yavuruga uuzaji wa chai ya Kenya
Mar 20, 2025 03:12Biashara ya chai ya Kenya imeingia matatani baada ya Marekani na Uingereza kuanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Yemen na kupelekea jeshi la Yemen kujihami na kujibu uvamizi wa madola hayo ya kibeberu.
-
Angola: Kilichokwamisha mazungumzo ya Jumanne baina ya serikali ya DRC na M23 ni nguvu za kigeni
Mar 20, 2025 03:11Wizara ya Mambo ya Nje ya Angola imesema kuwa mazungumzo ya amani kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi la March 23 ambayo yalipangwa kufanyika juzi Jumanne, yalisitishwa kutokana na ushawishi wa nguvu za nje.
-
AU yalaani shambulio dhidi ya msafara wa Rais wa Somalia
Mar 19, 2025 23:41Somalia na Umoja wa Afrika (AU) zimelaani shambulizi la kigaidi lililolenga msafara wa Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud huko Mogadishu, mji mkuu wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.