-
Waasi wa M23 wakataa kushiriki katika mazungumzo ya Luanda na serikali ya DR Congo
Mar 18, 2025 07:59Mazungumzo baina ya waasi wa M23 na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), yaliyopangwa kufanyika leo Jumanne huko Luanda, mji mkuu wa Angola, yamekwama baada ya kundi hilo la waasi kusema halitoshiriki.
-
Libya yaitaka jamii ya kimataifa kuisaidia mzigo wa wakimbizi
Mar 18, 2025 07:58Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya, Emad al-Tarabelsi, ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa ukiwemo pia Umoja wa Ulaya kuisaidia mzigo wa wakimbizi haramu wanatumia ardhi ya Libya kujaribu kuelekea barani Ulaya.
-
UN: Vita Ituri DRC vimepelekea watu 100,000 kuwa wakimbizi
Mar 18, 2025 04:18Umoja wa Mataifa unaripoti kuwa mapigano ya silaha katika jimbo la Ituri, Kaskazini-Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), yamesababisha watu takriban 100,000 kufurushwa kutoka makazi yao. Mapigano kati ya kundi la waasi wa M23 na Jeshi la Serikali ya DRC (FARDC) pia ni chanzo kuongezeka idadi ya wakimbizi katika jimbo la Kivu Kusini.
-
Rwanda yakata mahusiano ya kidiplomasia na Ubelgiji kutokana na mgogoro wa DRC
Mar 18, 2025 03:50Rwanda imekata mahusiano ya kidiplomasia na Ubelgiji Jumatatu huku kukiwa na mgogoro katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
-
RSF: Hatutoondoka Khartoum, Jeshi ndilo lililojitoa kwenye mazungumzo
Mar 17, 2025 22:43Kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraaka RSF vya Sudan amelilaumu jeshi la nchi hiyo SAF kwa kukwamisha mazungumzo ya amani nchini humo na kusema kuwa, askari wake hawataondoka mjini Khartoum.
-
Waziri wa Elimu Libya atupwa jela miaka 3.5 kwa ubadhirifu
Mar 17, 2025 22:42Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Libya imetangaza kwamba Waziri wa Elimu wa nchi hiyo, Musa al-Magaryaf, amehukumiwa kifungo cha miaka 3.5 jela kwa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.
-
Waasi wa M23 wasonga mbele zaidi mashariki mwa DRC kabla ya kuanza mazungumzo kesho Jumanne
Mar 17, 2025 08:26Waasi wa M23 leo wameendelea kushambulia maeneo mbalimbali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kabla ya kuanza mazungumzo ya moja kwa moja na serikali ya Kongo hapo kesho katika mji mkuu wa Angola, Luanda.
-
Mashambulizi ya RSF magharibi mwa Khartoum yauwa raia 4 na kujeruhi wengine 30
Mar 17, 2025 08:23Mamlaka ya serikali za mitaa huko Sudan imetangaza leo Jumatatu kuwa mashambulizi ya mizinga ya wanamgambo wa kikosi cha RSF yameua raia wanne na kujeruhiwa wengine 30 katika mji wa Omdurman unaopatikana katika jimbo la Khartoum, mji mkuu wa nchi hiyo.
-
Kagame akosoa kimya cha Magharibi kuhusu FDLR; aisuta Ubelgiji
Mar 17, 2025 08:11Rais wa Rwanda, Paul Kagame amezikosoa vikali nchi za Magharibi kwa kueneza 'simulizi potofu' kwamba Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Angola yataka kusitishwa mapigano kabla ya mazungumzo ya amani DRC
Mar 16, 2025 22:55Rais wa Angola, João Lourenço, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano katika mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).